Merkel asema milango itabaki wazi | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.07.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Merkel asema milango itabaki wazi

Wakati akizungumza na waandishi habari leo Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amepuuza miito inayomtaka kubadilisha msimamo wake wa kuwakaribisha wakimbizi licha ya kutokea mashambulizi kadhaa ya kinyama nchini humo.

Angela Merkel Porträt

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani

Katika mkutano wake wa kila mwaka na waandishi habari leo, Merkel alisema , wakati akijibu maswali juu ya kwanini hajatembelea maeneo ya matukio ya mashambulizi , na kusema tu kwamba atahudhuria sala ya kumbukumbu siku ya Jumapili mjini Munich kwamba anaamini hatua alizochukua ni sahihi.

Angela Merkel Bundespressekonferenz

Kansela Angela Merkel

Merkel ambaye alikatisha likizo yake ya majira ya jotoili kuweza kuzungumza na vyombo vya habari mjini Berlin, leo,(28.07.2016) amesema mashambuliaji manne katika muda wa wiki moja , "yanashitua, yanadhalilisha na yanachosha" lakini sio ishara kwamba maafisa wamepoteza udhibiti.

"Ukweli kwamba watu wawili ambao waliingia nchini Ujerumani kama wakimbizi wanahusioka na mashambulio manne mjini Wurzburg na Ansbach wanaikejeli nchi iliyowachukua. Na ningependa kuongeza kwamba hakuna umuhimu kabisa , hata kama watu hawa wawili waliwasili pamoja na wakimbizi wengine wengi kabla ama baada ya Septemba 4 mwaka jana."

Deutschland Olympia Einkaufszentrum in München Hauptbahnhof Polizei

Shambulio katika eneo la maduka la Olimpia mjini Munich

Wajerumani wataendelea kuwa tayari kuwapokea wageni

Kiongozi huyo wa Ujerumani amesema washambuliaji "walitaka kukandamiza hisia zetu za kijamii, uwazi wetu na kuwapo kwetu tayai kuwasaidia watu wenye shida."

Merkel alikuwa akizungumza baada ya shambulio la shoka, visu, mashambulizi ya risasi na shambulio la kujitoa muhanga kuiacha Ujerumani katika bumbuazi , na kusababisha watu 13 , ikiwa ni pamoja na washambuliaji hao kufariki na wengine darzeni kadhaa kujeruhiwa.

Deutschland Messerattacke am Grafinger Bahnhof

Shambulio katika treni karibu na Wurzburg

"Sheria ya juu kabisa ni kwamba panapotokea mgawanyiko, ni lazima tuchukua hatua kama tulivyokwisha fanya hadi sasa, ili iwe wazi kwamba tutafanya kila linalowezekana kibinadamu kuhakikisha usalama katika taifa letu huru na la kidemokrasia."

Merkel ameongeza kwamba hataruhusu wapiganaji wa Jihadi , kufuatia mashambulizi kadhaa yaliyosababisha maafa , nchini Ufaransa, Ubelgiji, Uturuki na katika jimbo la Marekani la Florida pamoja na Ujerumani , kuiweka serikali yake kushindwa kuongozwa na sababu za msingi pamoja na uelewa.

Amoklauf mit zwei Toten in Franken

Shambulio lililotokea Ansbach nchini Ujerumani

Wakati tabaka la kisiasa nchini Ujerumani limetoa wito kwa kiasi kikubwa kuwa na utulivu, vyama vya upinzani na waasi kutoka katika kundi la kisiasa la kihafidhina vimemshutumu kwa kuiweka wazi nchi hiyo kuwa katika hatari ya kushambuliwa bila ya kuwa na udhibiti imara wa watu wanaoingia.

Mashambulio nchini Ujerumani yamefanyika wakati uchaguzi katika majimbo mawili unakaribia mwezi Septemba, mjini Berlin na Mecklenburg magharibi.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / dpae

Mhariri: Josephat Charo

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com