1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel akutana na viongozi wa mashirika matano ya kiuchumi

CharoJosephat6 Februari 2009

Sheria mpya kuundwa

https://p.dw.com/p/GoVz

Kansela wa Ujerumani bi Angela Merkel ametoa mwito wa kuwepo muelekeo mpya wa kiuchumi huku ulimwengu ukikabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi. Kiongozi huyo ametoa mwito huo pamoja na viongozi wa mashirika matano ya kiuchumi baada ya mkutano wao mjini Berlin hapa Ujerumani hapo jana.

Kansela wa Ujerumanai Angela Merkel alikutana na viongozi wa shirika la fedha la kimataifa, IMF, shirika la biashara la kimatiafa, WTO, benki ya dunia, shirika la OECD na shirika la kazi la kimataifa, ILO kwenye makao yake mjini Berlin kujadili njia za kushirikiana katika kukabiliana na mpromoko mkubwa wa kiuchumi duniani.

Baada ya mkutano wao viongozi hao walitoa taarifa ya pamoja kuhimiza hatua muafaka zichukuliwe haraka na muungano wa nchi 20, G20, kuzifanyia marekebisho sheria kuhusu fedha, kuyamaliza kwa ufanisi mazungumzo ya Doha kuhusu biashara ya kimataifa na juhudi za kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa na kuangamiza umaskini. Katibu mkuu wa shirika la kimataifa la ushrikiano wa kibishiara na maendeleo, OECD, Angela Guria amempongeza kansela Merkel akimataja kuwa mfano mzuri wa kiongozi mwenye stahamala.


O-Ton Gurria

''Ningependa kusema tuko mbele ya mfano mzuri wa uongozi. Mabadiliko hutokea sio tu kwa sababu viongozi wana maoni yaliyo wazi lakini pia huvumilia.''


Hapo kabla kansela Merkel alitaka kuwepo sheria mpya za kimataifa kuhusu uchumi. Wazo lake sasa limeungwa mkono na viongozi wa mashirika matano ya kiuchumi duniani na kutaundwa sheria zinazolenga kuwepo maendeleo ya kiuchumi ya kudumu. Kansela Merkel amesema itakuwa muhimu kutozisahau nchi zinazoendelea wakati wa mgogoro huu wa kiuchumi.


O-ton Merkel

''Nchi zinazoendelea hazina tu haki ya usawa wa kimaendeleo, bali pia katika masilahi yetu tunataka kuwepo maendeleo mazuri ya pamoja. Kwa sababu maendeleo ya kiuchumi hayawezi kwa kipindi Kirefu kupatikana bila kuzishirikisha nchi zinazoendelea.''


Katibu mkuu wa shirika la biashara la kimataifa, WTO, Pascal Lamy, ameelezea wasiwasi wake juu ya nchi zinazoendelea kuhusiana na viwango vikubwa vya fedha zinazotolewa na serikali mbalimbali kusaidia uchumi wao.


O-Ton Lamy

'' Mipango hii yote ya kusaidia uchumi, viwango hivi vya fedha za umma zinazonuiwa kupewa mabenki au viwanda huenda vikasababisha athari zitakazovuruga biashara.''


Muongozo wa sheria mpya kuhusu uchumi endelevu uliofikiwa baada ya mkutano wa kansela Merkel na viongozi watano wa mashirika ya kiuchumi ya kimataifa, unatakiwa kuboresha utandawazi. Ili kuzuia migogoro ya kiuchumi ya aina hii katika siku za usoni, lazima hatua zote za kisiasa ziratibiwe kwa pamoja, anasema Dominique Strauss-Kahn, kiongozi wa Fuko la Fedha la kimataifa.


O-Ton Strauss-Kahn

''Hiyo ndiyo sababu swala la utawala wa jinsi tunavyoweza kuratibu njia mpya ya kusimamia sio tu sekta ya fedha, bali pia uchumi wa dunia, ni swala lenye umuHimu mkuwa leo.''


Mkutano kati ya kansela Merkel na viongozi hao watano wa mashirika ya kimataifa umefanyika wakati serikali mbalimbali zikichukua hatua za kuzisaidia benki zao na kuanzsiah sheria mpya kupunguza matumizi mabaya ya fedha ambayo yamesababisha mgogoro huu mbaya wa kiudhumi kuwahi kutokea.