Merkel aisifu Jordan kwa kuwahifadhi wakimbizi wa Syria | Matukio ya Kisiasa | DW | 21.06.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Merkel aisifu Jordan kwa kuwahifadhi wakimbizi wa Syria

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema mataifa ya Umoja wa Ulaya yana wasi wasi kuhusu mpango wa makombora wa Iran na kutoa wito kupatikana suluhisho la vitendo vya uchokozi wa Iran katika mashariki ya kati.

Vitendo  vya  uchokozi vya  Iran  sio  tu  vinahitaji  kujadiliwa, lakini tunahitaji  suluhisho  la  haraka," alisema  kansela  Merkel  baada  ya kukutana  na  mfalme  wa  Jordan  Abdullah  mjini Amman.

Jordanien | Angele Merkel zu Besuch in Amman (Getty Images/AFP/A. Abdo)

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akilakiwa kwa heshima za kijeshi nchini Jordan

Ujerumani  itaendelea  kuwa sehemu  ya  makubaliano  ya  kinyuklia na  Iran, ambayo  yaliondoa  vikwazo dhidi  ya  nchi  hiyo  kwa kubadilishana  na  udhibiti  wa  mpango  wake  wa  kinyuklia, baada rais  wa  Marekani Donald Trump  kujiondoa   kutoka  mkataba  huo mwezi Mei  mwaka  huu.

Merkel  alisema  kwamba  wakati  nchi  za  mataifa  ya  Ulaya yanataka  kuendelea  na  makubaliano  hayo  yaliyfikiwa  mwaka 2015, mataifa  hayo  yana  wasi  wasi  kuhusu mpango  wa makombora  wa  Iran, kuwapo  kwake  nchini  Syria  na  jukumu  lake katika  vita  nchini Yemen.

Kansela  Merkel aliwasili  nchini  Jordan kama  sehemu  ya  ziara yake  ya  siku  mbili  ambayo  pia  itamfikisha  nchini  Lebanon , nchi mbili ambazo  zimeathirika  mno na  mzozo  unaoendelea  nchini Syria.

Bundeskanzlerin Merkel in Jordanien (Reuters/M. Hamed)

Kansela wa Ujerumani alipohutubia chuo kikuu cha Ujerumani na Jodran mjini Amman

Merkel aipongeza Jordan  

Pia  ameipongeza  Jordan  kwa  kuwapokea  wakimbizi  wa Syria. Nchi  hiyo  ya  kifalme imewapokea  wakimbizi  karibu 650,000 kutoka  Syria. Kuhusu  sera  ya  kufungua  milango  kwa  wakimbizi nchini  Ujerumani, kansela  amesema  mazungumzo  yanaendelea kuhusu  sea  bora  zaidi, lakini  hakuna  shaka  ya  kufunga milango.

"Nadhani kwa  kiasi  kikubwa  hakuna  haja  ya  kuwa  na  hofu , na  bila  shaka  naweza  kusema  hakuna  mtu anayeweza kufunga mipaka. Na  kwa  kiasi  kikubwa  Ujerumani  ni  salama, licha  ya  kuwa  kunatokea  matukio  ambayo  shutuma hutupwa  kwa  wageni  kwa  mashambulizi. Lakini  pia  kuna wakati wakimbizi  hasa  wanawake wameuwawa. Kwa  hiyo shutuma zinakwenda  kwa  pande zote."

Kansela  ameahidi mkopo  wa  dola  milioni  100  kwa  Jordan , ambako  maandamano  ya  hivi  karibuni  yamelazimisha  baraza  la mawaziri  kujiuzulu mwezi  huu  kuhusiana  na  hatua  za  kubana matumizi. Merkel  amesema  mkopo  huo, ambao  unakuja  baada  ya mkopo  mwingine  wa  euro milini 384 ambao Ujerumani uliiahidi Jordan mwaka  huu, una  lenga  kusaidia  juhudi  za  nchi  hiyo kutekeleza  mageuzi ambayo  yanatakiwa na  shirika  la  fedha  la kimataifa.

Bundeskanzlerin Merkel in Jordanien (Reuters/M. Hamed)

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel(kushoto) akiwa pamoja na mkurugenzi wa lugha wa chuo kikuu cha Ujerumani na Jordan mjini Amman Dorothea Jecht

mapema  leo, Merkel  alihutubia  wanafunzi  katika  chuo  kikuu cha Ujerumani  na  Jordan mjini  Amman , chuo  kikuu  cha  tatu  kikubwa nchini  Jordan, ambacho  kilianzishwa  mwaka  2005. Kiasi ya Wajerumani  100  wanashirika  katika  kukiendesha  chuo hicho na kuandika  mitaala  ya  chuo pamoja  na  ziara  ya  masomo  nchini Ujerumani  na  Austria. Merkel  pia  atakutana  na  wanajeshi wa Ujerumani  walioko Jordan  kama  sehemu  ya  muungano  wa  kijeshi unaoongozwa  na  Marekani  kupambana  na  wanamgambo  wa  kile kinachojulikana  kama  Dola  la  Kiislamu  nchini  Iraq  na  Syria.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / dpae

Mhariri: Iddi Ssessanga

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com