1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel aikosoa Kremlin

Mohammed Abdul-Rahman2 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVjR

Berlin:

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ameishitumu Ikulu ya Urusi-Kremlin- kwa kuvikandamiza vyama vya upinzani kabla ya uchaguzi wa bunge hii leo. Akizungumza katika mahojiano na redio ya umma ya Ujerumani, Kansela pia ameelezea kusikitishwa kwake kwamba hakuna waangalizi kutoka shirika la usalama na ushirikiano barani ulaya watakaokuweko kushuhudia uchaguzi huo. Pamoja na hayo amesisitiza kuwa ni muhimu kudumisha uhusiano mzuri na Urusi, akiongeza kwamba nchi hiyo ina mchango muhimu wa kutoa katika kutatua mzozo wa kimataifa kuhusu mpango wa nuklea wa Iran na mustakbali wa jimbo la Serbia la Kosovo.