Meneja wa Posta Zumwwinkel ajiuzulu | Matukio ya Kisiasa | DW | 15.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Meneja wa Posta Zumwwinkel ajiuzulu

Meneja wa kampuni ya Posta nchini Ujerumani bwana Klaus Zumwinkel ang'atuka.

Klaus Zumwinkel meneja wa Posta ang'atuka kutokana na tuhuma za kukwepa kodi.

Klaus Zumwinkel meneja wa Posta ang'atuka kutokana na tuhuma za kukwepa kodi.

Bwana Zumwinkel ambae sasa anafanyiwa uchunguzi na polisi anatuhumiwa kutorosha kiasi cha Euro milioni moja nje ya nchi.

Mtuhumiwa huyo bwana Klaus Zumwinkel amekuwa anatuhumiwa kutenda uhalifu wa kuepa kulipa kodi kwa muda wa miaka mingi.

Kwa mujibu wa tuhuma hizo meneja huyo alitorosha kiasi cha Euro milioni moja na kuzificha katika benki moja nchini Liechtenstein.

Mtuhumiwa anadaiwa kutenda uhalifu huo katika kipindi cha miaka 20 ili kukwepa kulipa kodi nchini Ujerumani.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amekaribisha uamuzi wa bwana Zumwinkel kujiuzulu.

Akizungumzia hatua hiyo, msemaji wa wizara ya fedhaa Torsten Albig ameeleza kwamba"Uamuzi wa bwana Zumwinkel kung'atuka unaungwa mkono na serikali ya Ujerumani."

Wadadisi wanasema mkasa wa meneja huyo huenda ukageuka kuwa kashfa kubwa na kuwahusisha watu wengi.

Polisi ya Ujerumani imesema wafanya biashara karibu mia saba pamoja na wasanii wa burdani wa Ujerumani wanafanyiwa uchunguzi kuhusiana na tuhuma zinazomkabili bwana Zumwinkel. Na kwa mujibu wa shirika la habari la AP benki moja ya nchini Liechtenstein pia inafanyiwa uchunguzi

Juu ya tuhuma za kutenda uhalifu bwana Zumwwinkel mwenyewea ameesema"Nimezaliwa Rheinland Palatinate, na nafurahi kwamba naweza kuishi kwa furaha na kulipa kodi."

Nyuymba na ofisi za bwana Zumwinkel zimefanyiwa msako na polisi pamoja na maafisa wa idara ya fedha.Hatahivyo mtuhumi wa huyo yupo nje kwa dhamana.

Kutokana na tuhuma zinazomkabili bwana Zumwinkel, wanasiasa wa Ujerumani wametoa mwito juu ya kubadili sheria zinazohusu kuwaadhubu watu wanaoepa kulipa kodi.

Wakati huo huoKansela Angela Merkel amemtaka bwana Zumwinkel ajieleze hadharani kwa manufaa yake na wafanyakazi wote wa kampini ya posta.

Bwana Zumwinkel alihesabika miongoni mwa mameneja waliokuwa na mafanikio makubwa nchini Uejrumani.

Ameiongoza kampuni ya posta tokea mwaka 1990 yenye wafanyakazi nusu milioni.

.......... • Tarehe 15.02.2008
 • Mwandishi Wenkel, Rolf (DW)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D8AV
 • Tarehe 15.02.2008
 • Mwandishi Wenkel, Rolf (DW)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D8AV
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com