MELI YAZAMA,ZAIDI YA 200 WAFA | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 10.09.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

MELI YAZAMA,ZAIDI YA 200 WAFA

Watu zaidi ya 200 wamekufa katika ajali ya meli nchini Tanzania.

default

Waokoaji wakioandoa maiti za watu waliokufa baada ya meli kuzama kisiwani Zanzibar

Watu zaidi ya 200 wamekufa baada ya meli kuzama kisiwani Zanzibar.

Meli hiyo iliyokuwa inaekelea kisiwani Pemba kutokea Unguja ilikuwa na abiria zaidi ya 600.

Shirika la msalaba mwekundu limetoa taarifa hiyo. Miongoni mwa waliokufa walikuwa wanawake na watoto. Taariza zaidi zinasema kuwa watu zaidi ya 325 waliokolewa.

Sababu ya kutokea ajali hiyo haijajulikana. Lakini baadhi ya abiria wamelalamika kuwa meli iyo ilikuwa imejaa sana. Meli hiyo "MV Spice Islander" iliyokuwa imejaa sana ilizama leo alfajiri ikiwa njiani kuelekea kisiwani Pemba. Ilikuwa imejaa abiria,shehena ya mchele na bidhaa nyingine.

Rais wa Ujerumani Christian Wulff, kwa niaba ya Wajerumani wote , amemtumia Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania salamu za rambi rambi kwa msiba huo.

i

 • Tarehe 10.09.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/12WiL
 • Tarehe 10.09.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/12WiL

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com