Tunatumia 'cookies' ili kuboresha huduma zetu kwako. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana katika sera yetu ya faragha.
Wahanga wa uhalifu wa Ntaganda kulipwa fidia dola milioni 30/ HRW yataka Burundi kuwaachilia wahamiaji wanaoshikiliwa/ Ousmane Sonko atoa wito wa maandamano zaidi Senegal/ Ujerumani: Wabunge wawili wamelazimishwa kujiuzulu/ Marekani yalaani shambulio la kundi la waasi wa Houthi dhidi ya Saudi Arabia
Siku ya Mwanamke ulimwenguni / Kesi dhidi ya Chauvin yaanza kusikilizwa/ Muungano wa kijeshi nchini Yemen wafanya mashambulio dhidi ya waasi wa Houthi/ Meghan Markle aungwa mkono kuibuwa ubaguzi kwenye Ufalme wa Uingereza
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amekutana na kiongozi wa waislamu wa Shia nchini Iraq. Ujerumani imesema uondoaji vikosi vya kigeni nchini Afghanistan ufanyike kwa tahadhari. Côte d'Ivoire inafanya uchaguzi wa bunge hii leo.
Serikali ya Tanzania imetoa onyo kali dhidi ya wale wanaotoa na kusambaza taarifa kuhusiana na magonjwa ya mlipuko ikiwamo janga la maambukizi ya virusi vya corona// Papa Francis ziarani Iraq// Akiwa ziarani mjini Kinshasa David Beasly amesema WFP itaendesha miradi ya kusambaza misaada kufuatia uhaba wa chakula.
Mawaziri walioapishwa ni wawili kutoka ACT - Nassor Ahmed Mazrui na Omar Said Shaaban, na Dk. Saada Mkuya kutoka CCM// Kenya-Waandishi habari wanne na mbunge wameshambuliwa katika vurugu zilizoukumba uchaguzi mdogo waeneo la London, Nakuru// ICC yaanza kuchunguza uhalifu katika maeneo ya Wapalestina// Ujerumani kulegeza kwa hatua vizuizi vya COVID-19.
Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani pamoja na jeshi la Iraq wamethibitisha kwamba kituo cha kijeshi kinachotumiwa na muungano huo kimeshambuliwa kwa makombora yapatayo kumi upande wa magharibi mwa Iraq hivi leo// Kanisa Katoliki nchini Tanzania limesema mapadre wake wapatao 25 wamefariki dunia katika kipindi cha miezi miwili iliyopo// Kenya yapokea chanjo ya corona.
Wanafunzi 279 waliotekwa nyara Nigeria waachiwa huru// Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi leo amemuapisha Makamo wa kwanza wa Rais, Othman Masoud Othman Ikulu mjini Zanzibar// Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mkutano wa Kitaifa wa Maaskofu wa Kongo (CENCO) umeonya kuwa raia hawatavumilia uchaguzi kuahirishwa.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ndiye mwenyekiti mpya wa EAC/ Hali ya COVID 19 ikoje mpakani mwa Burundi na Tanzania?/ Human Rights Watch yataka Sudan ikomeshe kamatakamata/ Suu Kyi afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka mapya/ Trump afikiria kuwania tena Urais 2024
Israeli yatakiwa kusimamisha ubomoaji wa makazi ya Wabedouin katika Bonde la Jordan, waziri wa mambo ya nje wa Bangladesh A.K. Abdul Momen asema nchi yake haina wajibu wa kutoa hifadhi kwa wakimbizi 81 wa jamii ya waislamu ya Rohingya na Saudi Arabia yakanusha ripoti ya Marekani kuwa mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo Mohammed bin Salman aliidhinisha mauaji ya Jamal Khassogi
Chama cha ACT Wazalendo nchini Tanzania, kimeanza vikao vyake vya ndani, kumchagua mrithi wa Maalim kama makamu wa rais// Mauaji ya balozi wa Italia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamezusha mvutano kati ya nchi hizo mbili// Marekani kutoa ripoti kuhusu mauaji ya Jamal Khashoggi// Jeshi la Marekani limefanya mashambulizi ya anga kwenye maeneo ya mashariki mwa Syria.
Licha ya serikali ya Tanzania kukiri kuwepo kwa janga la virusi vya corona nchini humo, viongozi wengi wakiwemo mawaziri wameendelea kupuuza umuhimu wa kuvaa barakoa. Wananchi wasema wanaonesha mfano mbaya// Chama cha riadha nchini Kenya, kimewazuia wanariadha wake kwenda kushiriki mashindano makubwa ya riadha ya Tanzania (Kilimanjaro Marathon).
Magufuli awaonya makandarasi wanaochelewesha miradi ya serikali/ Kenya: kaunti 39 zimeidhinisha mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020/ Biden, Trudeau wakuza mahusiano ya Marekani na Canada/ Mahakama ya Ujerumani yamhukumu afisa wa zamani wa Syria/ Yemen yaonya wimbi jipya la COVID-19
Corona: Tanzania na Zanzibar zavunja kimya chao/ Marekani yapoteza nusu milioni kwa COVID-19/ Serikali ya Kongo imelaani shambulizi lililofanyika na kusababisha kifo cha balozi wa Italia nchini humo na inaahidi kufanya uchunguzi wa kina/ Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya, zimeihimiza serikali ya Somalia na upinzani kukubaliana kuhusu tarehe ya uchaguzi
Hatimaye Magufuli akiri Tanzania ina tatizo la COVID-19/ Kabila kupelekewa polisi wa kawaida. Siku moja baada ya hatua hiyo ameonekana akielekea Dubai> Mahojiano/ Tanzania: Kufunga shule eneo la Longido kufuatia hatari ya kuvamiwa na nzige/ Iran, IAEA wafikia makubaliano ya muda kuhusu nyuklia/ Umoja wa Mataifa walaani matumizi ya nguvu Myanmar
Zanzibar- Viongozi wa ACT Wazalendo waelezea kauli na wasia wa marehemu Maalim Seif Sharif kabla ya kifo chake// Wakenya 9 kati ya 10 wanasema hali yao ya uchumi itadorora zaidi iwapo ugonjwa wa COVID-19 utaendelea kuenea// Chanjo zaidi ya 11,000 kupelekwa Guinea kukabiliana na ebola// Milio ya risasi imesikika na makombora yamelipuka leo Ijumaa katikati mwa mji wa Mogadishu
Mwanasiasa mkongwe wa visiwani Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, anazikwa leo hii kwenye kijiji alichozaliwa cha Mtambwe kisiwani Pemba// DR Congo- Kumeanzishwa na kampeni ya chanjo dhidi ya homa ya Ebola katika mji wa Butembo// Rais Joe Biden wa Marekani amezungumza kwa simu na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ikiwa ni mara ya kwanza kwa viongozi hao na kujadiliana kuhusu ushirikiano.
Makamu wa rais wa Zanzibar Maalim Seif afariki dunia/ Mahakama ya Rwanda imeanza leo kusikiliza kesi dhidi ya meneja wa zamani wa hoteli ya Mille Collines mjini Kigali, Paul Rusesabagina/ Umoja wa Mataifa waonya kuhusu vurugu Myanmar
Sama Lukonde Kyenge ateuliwa Waziri Mkuu mpya wa DRC/ Viongozi wa G5 wafanya mkutano kujadili vita dhidi ya ugaidi/ Jeshi la Myanmar ladai kwamba halikuipindua serikali Licha ya kufutiwa mashitaka,Trump bado aendelea kuandamwa/ Mataifa masikini kuanza kupelekewa chanjo dhidi ya COVID-19
Rais wa Marekani amesema demokrasia imedhoofika baada ya Seneti kushinda kumtia hatiani Donald Trump. Maelfu ya watu wameendelea na maandamano ya kupinga utawala wa jeshi nchini Myanmar. Afghanistan inajaribu kudhibiti moto uliosababishwa na kuripuka kwa lori la mafuta.
Maandamano ya kupinga mapinduzi ya kijeshi Myanmar yanaendelea kwa siku ya nane. Mario Draghi kuapishwa kama waziri mkuu mpya wa Italia. Na, Zimbabwe yajiandaa kupokea chanjo laki 8 za COVID-19.