Tunatumia 'cookies' ili kuboresha huduma zetu kwako. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana katika sera yetu ya faragha.
Karibu katika matangazo ya asubuhi ya DW Kiswahili
Karibu usikilize makala za Mtu na Mazingira // Utamaduni na Sanaa // Yasemavyo magazeti ya Ujerumani kuhusu bara la Afrika // Sura ya Ujerumani // Jukwaa la Manufaa // Je Umeipata Hiyo
Ivory Coast yajiandaa kwa uchaguzi muhimu wa bunge. Watetezi wa haki za wanawake katika mkoa wa Kivu kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walalamika juu ya unyanyasaji na mauaji ya wanawake wakongwe, wanaohusishwa na uchawi. Ni wikiendi nyingine ya michuano ya Soka la Ujerumani Bundesliga.
Kwa mara ya kwanza kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis anakwenda nchini Iraq wiki hii// Shirika la waandishi habari wasiojali mipaka limepeleka malalamiko kwa waendesha mashtaka wa serikali ya Ujerumani, wakimtuhumu mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Marekani yasema uhusiano wake na China ni mtihani mkubwa// Macron akiri kuwa Ufaransa ilimuua mpiganiaji wa uhuru nchini Algeria// Ujerumani yarefusha vikwazo vya Covid-19 hadi Machi 28
Baraza la Usalama la UN kukutana kuzungumzia juu ya kadhia ya Myanmar//Marekani na Umoja wa Ulaya wawaekea vikwazo maafisa wa Urusi//Macron aitaka Iran kuonyesha "ishara wazi" juu ya ukaguzi wa nyuklia
Guterres asikitishwa na kiwango kidogo cha msaada kuisaidia Yemen/WHO yaonya juu ya kuweka matumaini yasio ya ukweli kuhusu kukamilika kwa Covid-19/Myanmar: Marekani yataka jamii ya kimataifa kuongeza shinikizo kwa jeshi la Myanmar
Watu 18 wauawa katika maandamamo Myanmar Trump: Huenda nikawania tena Urais 2024 Rais wa zamani wa Ufaransa kujua hatma yake juu ya kesi ya ufisadi inayomkabili
Serikali ya Saudi Arabia yakanusha mwanamfalme Mohammed Bin Salmin kuagiza kuuliwa kwa Jamal Khashoggi. Syria na Iran zimelaani shambulizi lililofanywa na Marekani jana dhidi ya wapiganaji wenye silaha. Zaidi ya wafungwa 400 wametoroka jela nchini Haiti.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamesema vizuizi vya kupambana na janga la corona vinapaswa kuendelea. Rais wa Marekani Joe Biden amezungumza kwa mara ya kwanza na mfalme Salman wa Saudia Arabia. Waziri Mkuu wa Armenia apuuza miito ya kumtaka kujiuzulu.
Maafisa wa Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya wanasema safari ya mazungumzo na Iran kuhusu mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 itakuwa ndefu na ngumu// (Jamii ya Kikristo ya Iraq ni moja ya jamii kongwe na yenye madhehebu tofauti zaidi ulimwenguni, ikiwa na Wakaldayo, Orthodox ya Armenia, Waprotestanti na matawi mengine ya kikristo.
Leo ni siku ya mwisho katika siku saba zilizowekwa na Serikali ya Zanzibar kuomboleza kifo cha aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad / Tanzania: Chama cha ACT Wazalendo kinajiandaa kuanza mchakato wa kumsaka mrithi wa Maalim Seif Sharif Hamad/ Ujerumani ingependa kuwa na mahusiano mazuri na Ethiopia/ Mwanamume halisi project Kenya
Jumuiya ya kujihami ya NATO ilikubaliana kuongeza idadi ya wanajeshi wake nchini Iraq/ Janga la corona limeongeza mzigo wa dola trilioni 24 kwenye deni la dunia mwaka mmoja uliopita/ Kenya: Hitilafu ya umeme kusababisha zaidi ya twiga 14 kufariki mbugani Soysambu/ Watekaji nyara wenye uthubutu wanasababisha hofu ulimwenguni kote na haswa katika njia za bahari katika Ghuba ya Guinea
Kwenye matangazo yetu ya leo asubuhi tumekuandalia makala za Mazingira, Utamaduni na Sanaa, Makala ya Afrika katika magazeti ya Ujerumani, Mwangaza wa Ulaya, Jukwaa la manufaa na Je Umeipata hiyo?
Rais wa Marekani Joe Biden ahutubia mkutano wa kimataifa kuhusu usalama wa mjini Munich. Siku tatu baada ya kifo cha aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Wazanzibari wanatafakari hali itakuwaje siku za usoni. Niger kumchagua rais mpya siku ya Jumapili wakati ambapo rais wa sasa Mahamodou Issoufou, anakamilisha mihula yake miwili.
Rais wa Marekani Joe Biden leo atahudhuria kwa njia ya video mkutano wa kimataifa wa kila mwaka kuhusu masuala ya usalama mjini Munich Ujerumani// Kizazi kipya cha waandamanaji wanaodai demokrasia nchini Myanmar ni cha watu wa aina tofauti// Mafanikio ya Uganda katika kupambana na ugonjwa wa COVID 19 yamehusisha wanasayansi na matabibu wengi wanawake.
Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel ya mwaka 2018 Daktari Denis Mukwege anaeleza masikitiko yake kutokana na kuibuka tena kwa ugonjwa wa Ebola huko Butembo mashariki mwa nchi hiyo// Hatua ya serikali ya Uganda kusitisha elimu ya chekechea kwa muda usiojulikana imeibua mjadala miongoni mwa wananchi iwapo utawala huo unathamini ngazi hiyo ya elimu.
Rwanda: Kesi ya ugaidi dhidi ya Rusesabagina inaanza kusikilizwa leo/ Imetimia miaka 10 tangu kutokea wimbi la maandamano lililofuatiwa na mapinduzi yaliomng'oa madarakani kiongozi wa muda mrefu kanali Gaddafi nchini Libya/ Ngozi Okonjo-Iweala ameteuliwa kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya mkuu wa shirika la biashara la kimataifa WTO/ Burkina Faso: Watu milioni moja kuyakimbia makaazi yao
Libya imegawika tangu maandamano ya kutaka mageuzi yaliomuondoa madarakani dikteta Gadhafi/ Yemen: Licha ya shinikizo za Biden kuvimaliza vita, bado mchakato wa kuelekea kupatikana kwa amani ni mgumu/ Idadi inayoongezeka ya wanawake barani Afrika wanatumia huduma za uzazi wa mpango. Lakini viwango vya uzazi bado viko juu/ Mataifa ya Afrika magharibi yanashuhudia kuzuka tena kwa homa ya Ebola