Tunatumia 'cookies' ili kuboresha huduma zetu kwako. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana katika sera yetu ya faragha.
Rais wa Marekani Joe Biden atilia mkazo sheria za kuvaa barakoa na kuagiza kuwekwa chini ya karantini kwa watu wanaosafiri kuelekea nchini humo, viongozi wa Umoja wa Ulaya wawataka raia wa bara hilo kutosafiri kiholela na kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Umoja wa Ulaya, wasisitiza wito wa kuachiwa huru kwa kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny
Rais Biden ameyasaini maagizo ya kiutendaji yanayopinduwa yaliyokuwa yamewekwa na mtangulizi wake Donald Trump/ Kwa kutizama hatua ambazo ameanza kuzichukua na sera yake ya kigeni, afrika itegemee nini katika utawala mpya wa Marekani?// Mahakama kuu nchini Uganda itatoa maamuzi siku ya Jumatatu kama aliyekuwa mgombea urais Robert Kyagulanyi ana uhuru wa kutoka katika kizuizi cha nyumbani.
Kitendawili cha nani atakayekuwa kiongozi wa chama cha kihafadhina cha Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kimeteguliwa kufuatia ushindi wa Armin Laschet ambaye ni Waziri Mkuu wa jimbo la North-Rheine Westphalia, lililopo magharibi mwa Ujerumani. Sura ya Ujerumani inaangazia será ya Laschet ya mambo ya nje itakavyoweza kuwa kuelekea bara lake la Ulaya na pia barani Afrika. Harrison Mwilima asimulia
Makala ya Afya yako hii leo inaangazia ulemavu usioonekana ambao umekuwa ukuhusishwa na imani za kishirikina lakini kumbe ni ugonjwa wa kawaida. Mtayarishi na msomaji ni Anuary Mkama.
Mwaka mmoja umepita sasa na bado ni vigumu kuuvuka mto huu wa Sange baada ya daraja hili kukatika kutokana na mafuriko. Wanaoathirika zaidi na hali hii hasa ni madereva wa basi na malori yanayo peleka bidhaa kutoka Bukavu kuelekea Uvira. Tazama video hii iliyoandaliwa na Mitima Delachance.
Viongozi mbalimbali duniani wameendelea kutoa salamu zao za pongezi kwa rais mpya wa Marekani, Joe Biden// Maoni: Joe Biden ndiye Rais sahihi wa Marekani wakati huu// Visa vipya vya virusi vya corna vinavyojibadilisha vyazidi kuleta wasiwasi Ulaya//Congo imepiga hatua nzuri licha ya kuendelea kuwepo na makundi ya wapiganaji,amesema kiongozi wa Monusco,Leila Zerougui.
Nchini Marekani Joe Biden aliapishwa jana kuwa rais wa 46 pamoja na makamu wake wa rais Kamala Harris// Joe Biden ameshinda uchaguzi wa rais kwa sababu anaonekana kujali, wanasema wachambuzi// Kamala Harris ndiye makamu wa rais mpya wa Marekani. Yeye ndiye mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo, wa kwanza mwenye asili ya Afrika, wa kwanza mwenye asili ya India.
Joe Biden aapishwa kuwa rais wa 46 wa Marekani na kutangaza kuwa demokrasia imeshinda // Viongozi wa Umoja wa Ulaya kukutana leo kuzijadili changamoto zinazoongezeka za janga la corona // Na ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa waonya kuwa waasi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanajaribu kuuzingira mji mkuu Bangui
Trump aondokaa rasmi ikulu kwa mara ya mwisho kama rais/ Wachambuzi: Marekani iko katika hali ya mgogoro kiuchumi na hata kitamaduni. Joe Biden ameshinda uchaguzi wa rais kwa sababu anaonekana kujali/ Tanzania: Wanasiasa wa upinzani wameikaribisha hatua ya Marekani ya kuwaweka vikwazovya visa/ Uganda: Idadi ndogo sana ya wapiga kura imejitokeza kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa
Kashfa inayohusu mfumo wa mafao ya watoto nchini Uholanzi, imeilazimisha serikali nzima ya nchi hiyo kujiuzulu, katika uwajibikaji wa kisiasa.
Biden ataapishwa leo kuwa rais wa 46 wa Marekani/ Uganda baada ya uchaguzi: Waganda wenyewe wanasemaje kuhusu kile kilichotokea, hali ilivyo sasa na mwelekeo wa taifa hilo?/ Vyama vya upinzani katika Jamhuri ya Afrika ya kati vimeyapinga matokeo ya uchaguzi/ Kenya: Ongezeko la vijana wanaojiunga na makundi ya kigaidi
Wafuasi wengi wa Donald Trump wameihama mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter tangu Trump alipofungiwa akaunti zake, kwa madai ya kuwachochea baadhi yao hata wakavamia majengo ya bunge la nchi hiyo. Je, kampuni zinazomiliki majukwaa hayo zina haki ya kuwanyima watu uhuru wa kujieleza?
Kuelekea sherehe ya kumuapisha Joe Biden kama rais mpya wa Marekani, maandalizi yamekamilika ila sherehe hii si ya kawaida, kwanza kwasababu ya janga la virusi vya corona na pili kwasababu si kila Mmarekani ameridhika na Biden kuchukua hatamu za uongozi. Kwasababu hizo maadhimisho haya yatahudhuriwa na watu wachache mno kinyume na ilivyo ada na ulinzi umekuwa ni mkali mno.
Nasra Mbarak msichana wa umri wa miaka 26 jijini Mombasa, yeye ni mjasiriamala wa mitandio yaani Hijab. Ni biashara aliyoianza tangu akiwa shule ya msingi darasa la saba miaka 11 na moja iliyopita. Tazama video hii iliyoandaliwa na Faiz Musa.
Marekani: Rais mpya Joe Biden anaapishwa leo/ Hatua za dakika za mwisho za utawala wa Trump nchini Yemen, Iraq na Afrika Kaskazini zimekosolewa vikali. Lakini mara tu Biden atakapoingia madarakani, ni jinsi gani maamuzi hayo yanaweza kubatilishwa kwa haraka?/ FAO limeonya kwamba nchi kadha za eneo la upembe wa Afrika zinakabiliwa na kitisho kufuatia wimbi la tatu la nzige wa jangwani
Rais mteule wa Marekani Joe Biden kuapishwa leo chini ya ulinzi mkali // Ujerumani yarefusha muda wa utekelezwaji wa hatua kali za kuzuia janga la corona // Na makundi ya waasi yajikusanya viungani mwa mji wa Bangassou katika Jamhuri ya Afrika ya Kati
WHO yazilaumu nchi tajiri kwa kujilimbikizia chanjo za COVID-19/ Timu ya mawakili imewasilisha rufaa katika mahakama kuu ya Uganda ikitaka kuachiwa kwa aliyekuwa mgombea urais Robert Kyagulanyi pamoja mkewe Barbara Itungo/ Mazungumzo ya Rais Tshisekedi na wapinzani yakwama/ Ghasia zaendelea nchini Tunisia kwa siku ya nne mfululizo/ Dodoma: Ufunguzi wa maadhimisho ya lugha ya kiswahili
Usalama wa bahari unatajwa kuwa mashakani kutokana na shughuli za kibinadamu zinazohatarisha uhai wa viumbe baharini kuendelea kushuhudiwa katika mataifa mengi ulimwenguni hatua inayowatoa hadharani wataalamu wa mazingira na kutoa wito wa harakla kunusu uhai chini ya maji. Vidio na Hawa Bihoga #kurunzi
Mti wa Mgandi ambao ni sehemu ya matambiko katika jamii za kibantu, unaotumiwa pia kama dawa za kiasilia, uko katika hatari ya kukatwa. Wakaazi wa Ngoloka katika kaunti ya Kilifi nchini Kenya wanasema huenda hatua hiyo ikaharibu historia kubwa ya jamii hiyo. #Kurunzi19.01.2020
Mji mkuu wa pili nchini Kenya unafahamika kwa fukwe zake za bahari. Mwanamuziki Akeelah, anatutembeza katika paradiso hii iliyoko pwani ya Kenya.