Tunatumia 'cookies' ili kuboresha huduma zetu kwako. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana katika sera yetu ya faragha.
Marekani yataka jamii ya kimataifa kuongeza shinikizo kwa jeshi la Myanmar/Marekani yaitaka Saudi kuvunja kikosi chake cha mamluki/Makamu wa Rais wa Zimbabwe ajiuzulu kufuatia kashfa za ngono/Guterres asikitishwa na kiwango kidogo cha msaada kuisaidia Yemen
Guterres asikitishwa na kiwango kidogo cha msaada kuisaidia Yemen/WHO yaonya juu ya kuweka matumaini yasio ya ukweli kuhusu kukamilika kwa Covid-19/Myanmar: Marekani yataka jamii ya kimataifa kuongeza shinikizo kwa jeshi la Myanmar
Wazanzibari wamepokea vipi uteuzi wa Makamu wa kwanza wa Rais, Mhe. Othman Masoud anayeziba nafasi ya hayati Maalim Seif? Hawa hapa ni baadhi ya Wazanzibari waliozungumza na DW baada ya uteuzi huo. Video na Salma Said.
Othman Masoud Othman ameteuliwa kuwa makamo wa kwanza wa rais Zanzibar/ Ubadhirifu wa huduma za dawa katika hospitali za mikoa Tanzania/ Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy amehukumiwa na kifungo cha miaka mitatu/ Umoja wa Mataifa unakusudia kuchangisha dola bilioni 3.85 katika mkutano wa kimataifa wa wafadhili ili kuwaokoa mamilioni ya watu wa Yemen wanaokabiliwa na baa la njaa
Mashirika katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma huko Turkana, Kenya yanavyofanya kazi ya ziada kuboresha mazingira ya kambi hiyo. Mashirika hayo yanakusanya taka za plastiki ambazo baadaye zinatumika kutengeza bidhaa mbalimbali. Fuatana naye Michael Kwena katika video hii kufahamu zaidi
Sudi Mnette amezungumza na makamo mpya wa kwanza wa rais wa Zanzibar, mtu ambae mara zote ametajwa kuwa na misimamo isiyoyumba, Othman Masoud Othman. Ameshika wadhifa huo baada ya kifo cha aliyekuwa makamo wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad mwezi uliopita. Sikiliza
Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amehukumiwa na mahakama ya mjini Paris kifungo cha miaka mitatu. Atatumikia mwaka mmoja akiwa gerezani na miaka miwili akiwa nyumbani. Ni kutokana na mashtaka ya rushwa yaliyomkabili. Mchambuzi wa siasa Ahmed Rajab akiwa London amezungumza na John Juma, kwanza anaelezea uzito wa uamuzi huo.
Makala ya Afya yako inauangalia zaidi ugonjwa wa Msononeko tatizo la akili linalowaathiri watu wengi na inaongoza kwa ulemavu duniani kote na inachangia sana mzigo wa magonjwa ulimwenguni. Fathiya Omar amekuandalia makala hii
Deo Kaji Makomba amepata nafas ya kuzungumza na vijana waliothirika wa madawa ya kulevya walioko katika kituo cha kuwabadilisha Tabia cha Tasol mjini Dodoma, Tanzania. Je imekuaje wakaingia katika janga hili na wamefanikiwa vipi kujiokoa katika tatizo hili? Vijana Tugutuke inajibu masuali yote haya.
Katika kipindi hiki cha vijana mchaka mchaka Sylvia mwehozi anaangalia ajira tofauti kwa vijana zinazotokana na katika shughuli za harusi barani Afrika. Ni kwa kiasi gani kazi hizo zimeleta tofauti katika maisha ya vijana? Sylvia Mwehozi anakueleza zaidi.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ndiye mwenyekiti mpya wa EAC/ Hali ya COVID 19 ikoje mpakani mwa Burundi na Tanzania?/ Human Rights Watch yataka Sudan ikomeshe kamatakamata/ Suu Kyi afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka mapya/ Trump afikiria kuwania tena Urais 2024
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ndiye mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, akichukua mikoba hiyo kutoka kwa rais wa Rwanda Paul Kagame. Lakini changamoto katika jumuiya hiyo ni tele ikiwa ni pamoja na kushindwa kwa asasi zake, migawanyiko na hata kuhoji umuhimu wake. Zaidi John Juma amezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Dar es Salaam Abdulkadir Atiki.
Watu 18 wauawa katika maandamamo Myanmar Trump: Huenda nikawania tena Urais 2024 Rais wa zamani wa Ufaransa kujua hatma yake juu ya kesi ya ufisadi inayomkabili
Watu 18 wauawa katika maandamamo Myanmar//Trump: Huenda nikawania tena Urais 2024//Rais wa zamani wa Ufaransa kujua hatma yake juu ya kesi ya ufisadi inayomkabili
Watu 18 wauawa katika siku mbaya ya umwagaji damu Myanmar, Navalny kuanza kutumikia kifungo chake katika jimbo la Vladimir na Ufaransa yazungumza na Ujerumani kuhusu vizuizi vya usafiri vilivyotangazwa na Ujerumani baada ya wasiwasi wa kusambaa kwa ugonjwa wa COVID 19 katika eneo la ufaransa la Moselle.
Watu watano wameuwawa katika makabiliano ya polisi Myanmar, Wanaharakati 47 wakamatwa kwa makosa ya kufanya uasi Hong Kong na Rais wa Marekani Joe Biden kutoa tamko kuhusu Saudi Arabia siku ya Jumatatu
Karibu katika matangazo ya asubuhi ikiwa ni tarehe ya mwisho ya Mwezi Februari. Tumekuandalia makala za Mtu na mazingira, utamaduni na sanaa na nyinginezo
Marekani yaidhinisha chanjo ya tatu kwa matumizi ya dharura. Myanmar yamfuta kazi balozi wake wa Umoja wa Mataifa. Wanafunzi na walimu waliotekwa nyara kaskazini mwa Nigeria waachiwa huru.
Uamuzi wa rais Joe Biden wa kutomwadhibu mrithi wa mfalme wa Saudi Arabia kwa mauaji ya mwandishi habari Jamal Khashoggi wawavunja moyo wanaharakati, Iran yasema mashambulizi ya angani yaliofanywa Ijumaa na Marekani Mashariki mwa Syria yanachochea ugaidi na Spika wa bunge nchini Libya Aguila Saleh asema bunge kuzungumzia kura ya kutokuwa na imani na serikali mpya ya umoja wa taifa Machi 8
Israeli yatakiwa kusimamisha ubomoaji wa makazi ya Wabedouin katika Bonde la Jordan, waziri wa mambo ya nje wa Bangladesh A.K. Abdul Momen asema nchi yake haina wajibu wa kutoa hifadhi kwa wakimbizi 81 wa jamii ya waislamu ya Rohingya na Saudi Arabia yakanusha ripoti ya Marekani kuwa mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo Mohammed bin Salman aliidhinisha mauaji ya Jamal Khassogi