1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mechi za Ulaya zarudi chini ya changamoto ya corona

Bruce Amani
15 Februari 2021

Barcelona itakabana koo na Paris Saint-Germain katika Champions League huku ikiwa na kumbukumbu za mechi yao ya mwisho katika awamu hiyo hiyo miaka minne iliyopita

https://p.dw.com/p/3pNp6
Themenbild Liverpool darf für Leipzig-Spiel nicht einreisen
Picha: Dave Thompson/AP/dpa/picture alliance

Barcelona ya Lionel Messi itakabana koo Jumanne na Paris Saint-Germain katika Champions League huku ikiwa na kumbukumbu za mechi yao ya mwisho katika awamu hiyo hiyo miaka minne iliyopita ambapo Barca walipindua matokeo ya 4 – 0 na kushinda 6 -1 nyumbani. Staa wa PSG Neymar yuko nje kwa kuwa ni majeruhi na hatocheza dhidi ya timu yake ya zamani.

Mabingwa wa zamani Liverpool lazima waweke pembeni matatizo yao ya nyumbani watakapocheza dhidi ya RB Leipzig waliofika nusu fainali mwaka jana kwenye uwanja usiohusiana na timu zote mjini Budapest kutokana na kanuni za corona. Itakuwa mechi itakayowakutanisha makocha wawili mahiri wa Ujerumani Jurgen Klopp wa Liverpool na Julian Nagelsmann wa Leipzig. Siku ya Jumatano Sevilla itacheza dhidi ya Dortmund na Porto dhidi ya Juventus.

Vizuizi kuhusiana na aina mpya ya virusi vya corona vimelazimu mechi nane za mikondo ya kwanza na ya pili katika Champions League na Europa League kuchezwa katika nchi isiyofungamana na upande wowote. Kwa mujibu wa sheria za UEFA, klabu ya nyumbani lazima itafute uwanja usiofungamana na upande wowote.

Mwisho wa michezo kwa sasa. Kwa mengi Zaidi tembelea ukurasa wetu wa michezo, fungua dw.com/Kiswahili. Tupo pia kwenye mitandao ya kijamii tafuta DW Kiswahili na Bruce Amani

AFP, AP, DPA, Reuters