1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

Saninu Laizer apata jiwe jingine la tanzanite la kilo 6

Iddi Ssessanga
5 Agosti 2020

Mchimbaji mdogo nchini Tanzania aliegeuka tajiri katika usiku mmoja zaidi ya mwezi mmoja uliopita kwa kupata jiwe kubwa zaidi ya madini ya tanzanite, amechimba jiwe linge lenye uzito wa kilo sita.

https://p.dw.com/p/3gS2R
Tansania Miner zum Millionär | Saniniu Laizer
Picha: picture-alliance/AP Photo

Mchjimbaji mdogo nchini Tanzania alieamka usiku mmoja akiwa tajiri zaidi ya mwezi mmoja uliopita alipochimba mawe mawili kati ya makubwa zaidi ya madini ya tanzanite kuwahi kugunduliwa, ameangukiwa tena na bahati, kwa kuchimba jiwe la tatu lenye uzito wa kilo 6 linalokadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 2.

Mawe hayo matatu yaligunduliwa na Saninu Laizer. Mawe mawili ya kwanza yanakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 3.4.

Madini ya tanzanite, yenye rangi kali ya urujuani na samawati, yanakutikana nchini Tanzania tu, na yanazingatiwa kuwa mojawapo ya madini nadra sana duniani.  

Tansania Miner zum Millionär | Saniniu Laizer
Saninu Laizer, mchimbaji mdogo aliegeuka tajiri, mambo yake yanazidi kunyooka.Picha: picture-alliance/AP Photo

Laizer alipeperusha jiwe hilo kubwa kichwani kwake kabla ya kulikabidhi kwa maafisa wa serikali waliomkabidhi hundi kulinunua.

"Nawaomba wachimbaji wenzangu, kwamba tuwe wazalendo kwa kuheshimu sheria na kanuni na kujifunga wenyewe kufanyakazi kwa bidii ili tufanikiwe," alisema Laizer, akimaanisha kanuni kwamba madini ya tanzanite yanapaswa kuuzwa moja kwa moja kwa serikali, kuliko kwa wafanyabiashara haramu.

"Sisi Watanzania tumeamua kwamba madini yanapaswa kutunufaisha sisi kama taifa," alisema waziri wa madini Dotto Biteko. Tumeuza vya kutosha madini yetu kwa wengine wanaonufaika wakati jamii zetu zinasalia kuwa maskini. Kwa mfano, katika maeneo mengi ya uchimbaji biashara zimeongezeka. Hata maeneo ambako hakukuwa na biashara hivi sasa mambo yameboreka."

Chanzo: APE

Mhariri: John Juma