1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mchango wa mshikamano wawekewa suala la kuuliza

Oumilkher Hamidou26 Novemba 2009

Korti moja ya Niedersachsen yahoji uhalalifu wa watu kuendelea kuchangia katika fuko la kuijenga upya sehemu ya mashariki ya Ujerumani,miaka 18 baadae

https://p.dw.com/p/KgnK
Kwa mujibu wa mahakama mchango wa mshikamano ni kinyume na sheriaPicha: picture-alliance/dpa

Mchango wa mshikamano kwaajili ya ujenzi mpya wa sehemu ya mashariki ya Ujerumani na hatima ya kampuni la magari la Opel ndizo mada zilizohanikiza magazetini hii leo.

Tuanze lakini na mchango wa mshikamano,au "Soli" kama unavyojulikana humu nchini.Gazeti la "REUTLINGER GENERAL-ANZEIGER" linaandika:

Suala hapa sio kujipigania.Na wala hili si suala la kuoneana kijicho kati ya sehemu ya Magharibi na Mashariki-kwasababu wanaochangia katika fuko la mshikamano ni walipa kodi.Suala hapa ni kuhusu kuaminiwa wanasiasa.Na haiwezekani kuwaona wanasiasa wakiendelea kunga'ang'ania mchango huo kwasababu miaka nenda miaka rudi umekua ukimimina mabilioni katika makasha ya hazina ya serikali-ili kugharimia miradi jumla.Mchango wa mshikamano-Soli,lazma ufutwe.Naiwe kupitia hukmu ya korti ya katiba au la.Busara ya kisiasa itumike kutathmini kiwango cha mahitaji .Na ukweli ni kwamba,sisi walipa kodi,mabilioni yatakayopungua,tutalazimika kuchangia,naiwe kupitia mchango wa mshikamano-Soli au bila ya mchango huo."

Gazeti la Sächsischer Zeitung la mjini Dresden linahisi hata kama korti ya katiba ikiunga mkono uamuzi wa korti inayoshughulikia masuala ya fedha ya Niedersachsen,haitomaanisha mwisho wa dunia.Gazeti linaendelea kuandika:

Ni kiroja kuona kwamba ndio kwanza sasa,miaka 18 baada ya kuanzishwa,Soli inawekewa suala la kuuliza na jaji wa korti ya masuala ya fedha,kama mchango huzo uendelee kutolewa.Na hata kama korti ya katiba itaunga mkono hoja hizo,haimaanishi kua dunia ndio inamalizika.Kwasababu zile pesa ambazo miongoni mwa mengineyo,zinatumika kuijenga upya sehemu ya mashariki,zitabidi zikusanywe kupitia njia nyengine.Au waziri wa fedha atalazimika kufutilia mbali mpango ambao tokea hapo unazusha mabishano wa kupunguza kodi za mapato.

Gazeti la Darmstädter Echo" lina maoni sawa na hayo na linaandika.

Ikiwa kweli korti ya katiba mjini Karlsruhe itafutilia mbali mchango wa mshikamano,basi patahitajika njia nyengine ya kujipatia fedha hizo.Pengine walipa kodi watavunjika moyo.Lakini kufutwa moja kwa moja mchango wa mshikamano bila ya kuwepo njia mbadala,si jambo linaloingia akilini kwasababu ,itapelekea mfumo mzima wa sera za fedha kuvurugika.

GM verlegt Europa Zentrale nach Rüsselsheim
Makao makuu ya General Motors huko RüsselsheimPicha: picture-alliance/ dpa

Mada yetu ya mwisho inahusu kasheshe ya kampuni mama ya General Motor kuhusu matawi yake ya Opel nchini Ujerumani.Gazeti la FRÄNKISCHER TAG linaandika:

Baada ya kasheshe ya miezi kadhaa iliyopita,hatimae General Motors linaonyesha limeamua kweli kufanya marekebisho.:hatari lakini kwamba Opel linaweza kupotelewa na imani kuelekea kampuni mama la General Motors ,hivi sasa ni ndogo ikilinganishwa na hali namna ilivyokua mwaka uliopita.

Gazeti la NORDBAYERISCHER KURIER la mjini Bayreuth linaandika:

Msimamo usiokadirika wa General Motors unaweza kuendelea hivyo hivyo siku za mbele.Ingawa GM imeamua matawi yake ya Ujerumani na Ulaya yataendelea kuwepo.Lakini nini mameneja walioko Detroit watalazimisha kupatiwa badala yake kutoka kwa wanasiasa?Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya imejaribu kuzuwia mashindano ya kuania nafasi za kazi yasitokee miongoni mwa nchi za Ulaya.Lakini kama dhamiri za nchi kutoshindana wenyewe kwa wenyewe ni madhu,hakauna anaeweza kuashiria.

Mwandishi: Hamidou Oummilkheir /Inlandspresse

Mhariri:Aboubakary Liongo