1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbio za mwenge wa Olympik

Hamidou, Oumilkher10 Aprili 2008

Viongozi wa kamati kuu ya Olympic wazongwa na kizungumkuti cha mbio za mwenge

https://p.dw.com/p/Dfd5
Mwenyekiti wa kamati kuu ya michezo ya Olympik Jacques Rogge


Kamati ya kimataifa ya michezo ya Olympic IOC,ikikabwa na kizungumkuti cha machafuko wakati wa mbio za kuuzungusha mwenge wa Olympik duniani,imeitaka jamhuri ya umma wa China iheshimu ahadi iliyotoa ya kuimarisha hali ya haki za binaadam kabla ya michezo hiyo kuanza.Mwito huo haujakawia kujibiwa na viongozi wa mjini Beijing.


Mwenyekiti wa kamati ya kimataifa ya Olympic,Jacques Rogge amekiri mjini Beijing kwamba vugu vugu la Olympik linakumbwa na mzozo,lakini anasema "zamani"vizungumkuti vilikua vikubwa zaidi".Anaamini mzozo huu utatulia.


Baada ya machafuko yaliyofuatia mbio za mwenge wa Olympic jumatatu iliyopita mjini Paris,na baadae mbio hizo kugeuza njia San Francisco jana ili kukwepa kishindo cha wanaharakati wanaowaunga mkono Tibet,mwenyekiti wa kamati ya kimataifa ya Olympic Jacques Rogge amehakikisha hata hivyo mbio za mwenge za kuizunguka dunia zinaendelea hii leo,hazitasitisahwa,kesho itakua zamu ya Buenos Aires na jumapili mnwenge wa Olympik utafika Daresalam nchini Tanzania.


Jacques Rogge amewahakikishia wanariadha watakaoshiriki katika michezo ya Olympic ya msimu wa kiangazi-Austi ijayo mjini Beijing kwamba mzozo huu utasawazishwa na kuitaka China itekeleze ahadi ilizotoa kabla ya kukubaliwa kuandaa michezo ya olympic,"za kushughulikia zaidi masuala ya kijamii na hasa haki za binaadam.Mwenyekiti wa kamati ya kimataifa ya michezo ya Olympik Jacques Rogge anasema:


"Kuikubalia China michezo ya Olympic ni kwaajili ya kuimarisha ajenda ya masuala ya kijamii ikiwa ni pamoja na haki za binaadam.Kwa hivyo tunaitaka China iheshimu ahadi hizo za kiadilifu."


Tasngazo hilo halijakawia kujibiwa na viongozi wa mjini Beijing wanaoitaka kamati ya kimataifa ya michezo ya Olympik isiigeuze michezo ya Olympic kua ni suala la kisiasa.

"Nnaamini viongozi wa IOC wanaunga mkono michezo ya Olympic na wanajifungamanisha na muongozo wa Olympic unaokataza kujumuishwa masuala ya kisiasa katika michezo" amesema hayo msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje bibi Jiang Yu mjini Beijing.Ameongeza kusema tunanukuu"Nnataraji viongozi wa IOC wataendelea kujiambatanisha na muongozo wa Olympic mwisho wa kumnukuu.


Akihutubia mbele ya wawakilishi wa kamati 205 za Olympik za China wanaokutana mjini Beijing leo na kesho pamoja na kamisheni kuu ya IOC,Jacques Rogge ametoa hotuba kali akiwahimiza wawape moyo wanariadha kabla ya michezo ya olympic kuanza mwezi Agosti ujao.


"Wambieni,mambo yatabadilika baada ya mzozo huu wa sasa."Tumesaliwa na siku 120 na nnahakika tutafanikiwa."Amesema Jacques Rogger aliyesifu jinsi mbio za mwenge zilivyopita San Fransisco baada ya zahma za London na Paris.

Matumizi ya nguvu ya viongozi wa China dhidi ya waandamanaji wa Tibet mwezi uliopita yamezusha suala kama sherehe za ufunguzi za michezo ya Olympik zisusiwe au la.

Nao wabunge wa Ulaya waliokuatana hii leo,wamewatolea mwito viongozi wa Umoja wa Ulaya washurutishe kushiriki kwao katika sherehe hizo na kuanzishwa mdahalo kati ya viongozi wa mjini Beijing na mkuu wa kidini wa Tobet-Dalai Lama.

Wakati huo huo viongozi wa XChina wamepinga maobmi ya kamishna wa Umoja wa mataifa anaeshughulikia masuala ya haki za binaadam Louise Arbour ya kulitembelea jimbo la Tibet.


►◄