1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbio za kuwania nafasi ya waziri mkuu Japan zaanza

Sekione Kitojo
30 Agosti 2020

Katibu mkuu wa baraza la mawaziri la Japan Yoshihide Suga atajiunga na mbio za kurithi kiti cha mkuu wake Shinzo Abe kuwa waziri mkuu, vyombo vya habari vimesema leo Jumapili(30.08.2020).

https://p.dw.com/p/3hlus
Japan Premirminister Shinzo Abe erklärt Rücktritt
Shinzo Abe waziri mkuu wa JapanPicha: Reuters/F. Robichon

Mbio hizo zimepamba moto kuwania kiti cha waziri mkuu Abe ambaye ametumikia wadhifa huo akiwa kiongozi wa Japan ambaye  ametumikia  kwa muda mrefu zaidi.

Suga, mfuasi wa muda mrefu  wa  Abe  katika  jukumu  muhimu  la msaidizi , aliwahi  kukana kuwa  na  nia  ya  kiti  hicho lakini  alivutia shauku  kutokana na  mahojiano  kadhaa , na shirika  la  habari  la Reuters na  mashirika  mengine ya  habari, katika  siku  kadhaa kabla  ya  Abe  ghafla kutangaza  kujiuzulu kutokana  na  sababu  za kiafya.

Japans Regierung gibt Ära des künftigen Kaisers den Namen «Reiwa»
Yoshihide Suga katibu mkuu wa baraza la mawaziri la JapanPicha: Reuters/F. Robichon

Serikali  ya  Suga itaendeleza  mipango ya  bajeti na  kuchochea uchumi ambayo yalikuwa ni dira ya  utawala  wa  Abe  wa  karibu miaka minane  madarakani.

Tangazo la  Abe siku  ya  Ijumaa , akielezea  kuhusu kudhoofika  kwa hali  yake  ya  kiafya, iliweka  uwanja  wazi  kwa uchaguzi wa kiongozi  ndani ya chama cha  Liberal Democratic. Rais wa  chama cha  LDP ana  hakika  ya kuwa  waziri  mkuu  kwasababu  ya  wingi wa  wabunge  wa  chama  hicho  katika  bunge.

Suga aliamua  kujiunga  na  mbio za  kuwania kuwa  kiongozi  wa LDP akisema  anapaswa  kuchukua  jukumu  la  mbele kutokana  na matarajio  ya  uwezo wake wa  kushughulikia  matatizo, kama  janga la  COVID-19 pamoja  na  kuporomoka kwa  kiasi  kikubwa  uchumi wa  Japan tangu  vita  vikuu  vya  dunia, shirika  la  habari  la  Kyodo limesema, likinukuu chanzo  ambacho  hakikutajwa.

Kabinettsumbildung in Japan - Shinjiro Koizumi
Shinjiro Koizumi waziri wa mazingira wa Japan hatawania wadhifa wa waziri mkuu katika chama cha LDPPicha: picture-alliance/dpa/kyodo

Simu zilizopigwa  katika  ofisi ya  bunge  ya  Suga zikitaka  tamko kutoka kwake hazikupokelewa.

Suga atajiunga  na  wagombea  wengine  kama waziri wa zamani  wa mambo  ya  kigeni Fumio Kishida na  waziri wa zamani wa ulinzi Shigeru Ishiba.

Waziri wa mazingira Shinjiro Koizumi, mwenye umri  wa  miaka 39, mtoto  wa  waziri  mkuu  wa  zamani  Junichiro Koizumi  na anayefikiriwa  kuwa  waziri  mkuu  wa  baadae, ameamua  kutoshiriki katika  mbio  hizi, lakini atamuunga  mkono  waziri wa ulinzi Taro Kono, iwapo  atajiunga  na  mbio  hizo, kituo cha  taifa  cha  redio  na televisheni  , NHK kimesema.

Singapur  Shangri-la Dialogue Tomomi Inada
Waziri wa ulinzi wa Japan Tomomi Inada anataka kuwa waziri mkuu wa kwanza wa Japan mwanamkePicha: picture-alliance/AP/J. Nair

Waziri wa zamani  wa mambo ya ndani Seiko Noda na  waziri wa zamani wa ulinzi Tomomi Inada, ambaye anafahamika  kuwa mpenzi mno wa masuala ya bajeti, wanania  ya  kutaka  kuwa wanawake wa kwanza  nchini  Japan  kuwa  mawaziri  wakuu, vyombo  vya  habari vimeripoti.