Mazungumzo ya WTO huenda yasifaulu aonya Pascal Lamy | Habari za Ulimwengu | DW | 27.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Mazungumzo ya WTO huenda yasifaulu aonya Pascal Lamy

-

GENEVA

Kamishna mkuu anayehusika na masuala ya biashara katika Umoja wa Ulaya Peter Mandelson ameonya hii leo kwamba mwafaka katika mazungumzo ya kibiashara ya shirika la WTO huenda usifikiwe licha ya kuonekana dalili za maelewano kadhaa.

Bado nchi tajiri na zile maskini zinavutana kuhusiana na suala la ushuru wa bidhaa za kilimo.

India imechukua msimamo mkali katika mazungumzo hayo yanayoendelea dhidi ya Marekani Australia na nchi zingine zinazosafirisha bidha za kilimo kuhusiana na suala hilo la ushuru.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la biashara duniani WTO Pascal Lamy amependekeza kwamba nchi zinazoendelea kama India ziongeze ushuru katika bidhaa za kilimo kwa asilimia zaidi ya 15 nchi hizo zinasema kiwango hicho ni kitawaumiza wakulima wake.

Mawaziri wa biashara wamekuwa wakikutana tangu jumatatu kujadili juu ya punguzo la ruzuku na ushuru wa bidhaa za kusafirishwa kwa lengo la kutafuta njia za kufikia makubaliano mapya chini ya mazungumzo yanayojulikana kama duru ya Doha.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com