1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya Sudan na Sudan Kusini yaendelea

4 Septemba 2012

Sudan na Sudan Kusini zinaanza mazungumzo nchini Ethiopia ambayo yatarajiwa kuleta muwafaka wa kuweka ulinzi kwenye mpaka wao wa pamoja ili kuziwezesha nchi hizo mbili kuanza tena kusafirisha nje mafuta.

https://p.dw.com/p/16356
South Sudan’s chief negotiator, Pagan Amum (L) sits alongside Sudan’s Defence Minister Abdel-Rahim Mohamed Hussein (C), Sudanese spokesman Omer Dahab (R) as they announce that both countries have agreed to improve ties and cease hostilities during the latest round of talks in Addis Ababa on July 7, 2012. Sudan and South Sudan pledged to cease hostilities along their disputed oil-rich border Saturday but stopped short of actually signing an agreement, officials said. The verbal agreement came as the latest round of talks closed in the Ethiopian capital ahead of celebrations Monday to mark one year of independence for South Sudan.Negotiations resumed in May following weeks of deadly clashes along the oil-rich disputed border in April which brought the two rivals back to the brink of all-out war. The United Nations passed a resolution in May urging both sides to resolve outstanding disputes on oil sharing revenue and border demarcation by August 2. AFP PHOTO/JENNY VAUGHAN (Photo credit should read JENNY VAUGHAN/AFP/GettyImages)
Südsudan Amum Sudan Hussein Verhandlungen ArchivbildPicha: Getty Images/AFP

Sudan na Sudan Kusini zimekuwa zimekumbwa na msururu wa migogoro tangu Sudan Kusini ilipojitenga kutoka kwa jirani yake wa Kaskazini zaidi ya mwaka mmoja uliopita chini ya mkataba wa amani wa mwaka 2005. Mkataba huo ulimaliza miongo kadhaa ya vita.

Mapigano katika mpaka wenye umbali wa kilometa 1,800 yalitishia kuzitzmbukiza nchi hizo mbili katika vita kamili mnmo mwezi Aprili wakati Sudan Kusini ilipolichukuwa eneo tajiri la mafuta ambalo limedhibitiwa na Sudan kwa muda mrefu. Sudan Kusini ilifunga visima vyake vya mafuta mwezi Januari baada ya kushindwa kukubaliana na Sudan kuhusu ada inayostahili kulipa ili kusafirisha mafuta kupitia ardhi ya Sudan. Wanadiplomasia wan chi za Magharibi na wapatinishi wa Umoja wa Afrika sasa wanatarajia kukamilisha mazungumzo hayo baada ya nchi hizo mbili kukubaliana kuhusu mkataba wa mwanzo wa ada ya mafuta mwezi uliopita. Sudan inasema inataka mkataba wa usalama wa mpakani kabla ya usafirishaji mafuta kuanza tena.

Mpatanishi mkuu Thabo Mbeki ana matumaini pande zote mbili husika zitakubalina
Mpatanishi mkuu Thabo Mbeki ana matumaini pande zote mbili husika zitakubalinaPicha: Getachew Tedla Hailegiorgis

Maafisa kutoka pande zote wameelezea matumaini makubwa kuhusu mazungumzo hayo kuliko jinsi ilivyokuwa katika mazungumzo ya awali. Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za kigeni wa Sudan, El-Obeid Morawah, anasema ujumbe wa Sudan uko tayari kufikia makubaliano ifikapo mwishoni mwa awamu hii ya mazungumzo.

Mwenyekiti wa kamati ya masuala ya mpakani ya Sudan kusini, Michael Makuei Leúeth, anasema ana matumaini kuhusu kutatua masuala kama vile ya biashara ya mpakani, hali ya uraia katika nchi hizo mbili, pamoja na jimbo linalogombaniwa la Abyei. Anasema kuwa ikiwa serikali ya Sudan inakwenda kufanya mazungumzo kwa nia njema, basi kuna uwezekano wa kukubali kila kitu isipokuwa tu mipaka ambayo itafuata baadaye.

Visima vya mafuta Sudan Kusini kufunguliwa tena baada ya miezi sita
Visima vya mafuta Sudan Kusini vinatarajiwa kufunguliwa tena baada ya miezi sitaPicha: picture alliance / Tong jiang - Imaginechina

Pande zote mbili zinahitaji sana mapato ya mafuta ili kuanzisha tena uchumi wao. Mafuta yalikuwa yakitoa zaidi ya nusu ya mapato ya serikali nchini Sudan na kuchangia takribani asilimia 98 ya mapato ya serikali nchini Sudan Kusini kabla ya visima hivyo kufungwa. Nchi zote mbili zinakabiliwa na ughali wa maisha na uhaba wa fedha za kigeni zinazohitajika kulipia chakula kutoka ng'ambo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeweka Septemba 22 kuwa siku ya mwisho kwa nchi hizo mbili kutatua matatizo yao au zikabiliwe na vikwazo. atika kuanza, wapatanishi wanataka kujadili kuhusu kuwekwa eneo la amani mpakani lenye upana wa kilometa 10 ili kusaidia kuhakikisha kuwa upande wowote hauyasaidii makundi yenye silaha kuvuka mipaka, na kurejesha usafiri wa kawaida na bishara baina ya nchi hizo mbili.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters

Mhariri: Miraji Othman