Mazungumzo na Johh Nsambu | Matukio ya Kisiasa | DW | 11.03.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mazungumzo na Johh Nsambu

Waziri wa habari wa Uganda juu ya maonesho ya CEBIT na uhuru wa habari Uganda.

Mtoto mwanajeshi (Uganda)

Mtoto mwanajeshi (Uganda)

Waziri wa habari wa Uganda John Nsambu, alitembelea wiki hii Studio za Deutsche Welle mjini Bonn.Ziara yake hiyo ilifuatia kuhudhuria kwake maonesho ya ufundi wa kisasa na wa hali ya juu wa zana za mawasiliano ya habari CEBIT huko Hannover, mji mkuu wa Lower Saxony.

Nini Uganda imejifunza kutoka maonesho ya Cebit huko Hannover,ushirikiano katika sekta ya uenezaji habari kati ya Deutsche Welle na Uganda,uhuru wa habari nchi Uganda na hata vita vya kupambana na Jeshi la waasi la LRA na Joseph Konyi na iwapo Uganda wakati haukuwadia kuondoa majeshi yake nchini Somalia ni mada alizozungumzia. Wakati wa karamu maalumu huko Hannover, kandoni mwa maonesho ya CEBIT,waziri John Nsambu alikutana na Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani.

Ramadhan ali kwanza ,alimuuliza waziri John Nsambu aliejifunza katika Chuo Kikuu huko Braunschweig,Ujerumani ni umuhimu gani Uganda inaambatisha katika maonesho ya Teknolojia ya mawasiliano ya CEBIT huko Hannover:jibu lake:

"Tunaanza kutanabahi kuchukulia mambo juu juu tu,sio njia bora kwa nchi yoyote inayohitaji kuendelea ,kwani kila mtu popote pale akiwasili daraja fulani ya maendeleo au uwezo fulani wa kujimudu kifedhja hutaka kumiliki gari la aina ya Mercedes na "Mercedes" zaundwa Ujerumani bila ya kusahau magari mengine kama BMW.

Kwa jicho hilo utaona kila kitu kilichoundwa Ujerumani sio tu kina sifa ya juu n a urembo bali ni bidhaa pia ya kutegemea. "

Waziri wa habari wa wa Uganda akaongeza:

"Maonesho hayo ya teknolojia ya kisasa ya mawasiliano-ITC kwa bara la Afrika yaonesha ni chombo cha kutosogeza mbele ki- maendeleo na kwahivyo,

na chombo hicho lazima kiwe kiwe imara cha kutegemeka na bila shaka cha kuvutia."

Kwahivyo, kuja kwetu Ujerumani na kushiriki katika maonesho ya CEBIT ni kutafuta uwezekano wa kujipatia makampuni yalio ya kutegemeka kutusaidia katika sekta mbali mbali.

Kwahiyo tunazungumza na makampuni kama vile "BUNDESDRUKEREI" ili kutusaidia kuongoza mifumo yetu ya kuhifadhi dafutari.

Kuhusu vipi Uganda inashirikiana na nchi jiorani kimkoa mfano wa jirani zake Kenya na Tanzania,waziri Nsambu alisema:

"Mojawapo ya ushirikiano bora kabisa tulionao hivi sasa ni mpango wa waya maalumu-cable unaotokea Durban,Afrika Kusini hadi Mombasa na karibuni utatua Dar-es-salaam na Madagaskar na hata Visiwani Ceyschelles.Ceyschelles tayari inatumia. Utakapowasili katika bandari ya Mombasa, nchi kama Kenya na Tanzania zimo hivi sasa kuweka waya wao wa aina ya "Fibre Optic cable" na utakuwa kiungo kwa nchi zote 3 na hata pia Ruanda iliojiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini pia Burundi. "

Mradi huu ukianza kazi na imesalia miezi michache tu,mtandao wa Internet utakuwa wa haraka zaidi hata kushinda Ujerumani au Ulaya .Kwahivyo, kwa mara ya kwanza watakuwa na muundo-mbinu bora wa teknolojia ya hali ya juu,pengine kupindukia daraja ya Ulaya na hii inanifurahisha sana juu ya ushirikiano wao kati ya nchi za Afrika Mashariki-alisema waziri wa habari wa Uganda.

Ama kuhusu uhuru wa vyombo vya habari nchini Uganda,waziri wa habari John Nsambu alisema kuwa

uhuru wa habari nchini Uganda, nadhani aweza kudai kuwa, si nchi nyingi zinazoipita Uganda kwa kiwango kikubwa cha uhuru huo.Tatizo pekee analoliona waziri Nsambu,uhuru ambao vyombo vya habari vinapaswa kuwa nao : "uhuru wa vyombo hivyo kutoandika vitakavyo." Vyombo vya habari vyapaswa kuwaarifu watu yanayopita.Daima ilikua nia yake kurekebisha sheria ,kwani ukitoa uhuru kamili ,vyombo vya habari vitafanya vitakavyo,

Ni watu wanaohitaji vyombo vya habari asema waziri ili kujua kinapiti nini.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com