Mazungumzo juu ya kuvimaliza vita vya Ukraine yasimamishwa
19 Machi 2026
Msemaji wa serikali ya Urusi Dmitry Peskov, amewaambia waandishi wa habari kwamba Urusi inatumai duru mpya ya mazungumzo inaweza kufanyika baada ya hapo lakini Urusi imesema mazungumzo yake na Marekani kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na uwekezaji yataendelea.
Ukraine na Urusi, zimekuwa zinafanya vikao kwa upatanishi wa Marekani huko Abu Dhabi na Geneva mwaka huu, hata hivyo zinaendelea kutofautiana kuhusu msimamo wa Urusi wa kutaka kulidhibiti eneo lote la Donetsk.
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameyafafanua masharti ya Urusi ili kuvimaliza vita kwa kueleza kwamba Ukraine inapaswa kuachana rasmi, na azma yake ya kujiunga na NATO na kwamba ijiondoe kabisa kutoka kwenye maeneo manne ambayo Urusi inadai kuwa yake. Ukraine inapinga kuiachia sehemu hiyo ya ardhi yake ambayo inasema Urusi imeshindwa kuiteka.