Mazungumzo Cyprus yaingia hatua muhimu | Matukio ya Kisiasa | DW | 12.01.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mazungumzo Cyprus yaingia hatua muhimu

Mazungumzo kati ya pande mbili za Cyprus yameingia hatua muhimu na kuongeza matumaini kwamba nchi hiyo iliyogawika kwa miaka 43 huenda ikawa moja tena.

Wanadiplomasia wa juu kutoka Uingereza, Ugiriki na Uturuki wamejiunga na mazungumzo yanayoongozwa na Umoja wa Mataifa yanayonuwia kuiunganisha tena nchi iliogawanyika kwa muda mrefu ya Cyprus, wakati ambapo wapatanishi wanashughulikia masuala muhimu ya ulinzi wa kisiwa hicho cha mashariki mwa Mediterannia, ambako maelfu ya wanajeshi wa Uturuki wamewekwa katika upande uliojitenga wa kaskazini.

Kujiunga kwa mawaziri wa mambo ya nje wa uingereza Borris Johnson, Nikos Kotzias wa Ugiriki na Mevlut Cavusoglu wa Uturuki na mazungumzo hayo, kunamaanisha juhudi za miaka kadhaa za kuiunganisha tena nchi hiyo zimegusa usalama kwa mara ya kwanza. Suala hilo ni muhimu kwa makubaliano yoyote ya kumaliza mgawanyiko wa miaka 43, kwa sababu linagusia hofu miongoni mwa Wacyprus wenye asili ya Ugiriki na Uturuki.

Wakati mazungumzo hayo yakianza rais wa Cyprus ya Ugiriki Nicos Anastaciades alizungumzia uwezekano wa kuundwa kikosi cha polisi cha kimataifa, bila kueleza nani au namna gani kinawezwa kuundwa au kuongozwa, alisema mwandiplomasia aliehudhuria kikao hicho kwa sharti la kutotajwa jina kwa sababu haruhusiwi kutoa taarifa juu ya mazungumzo hayo.

Schweiz Zyperngespräche in Genf (Reuters/P. Albouy)

Kiongozi wa Cyprus ya Uturuki Mustafa Akinci akiwasili kwenye mazungumzo mjini Geneva, Jumatatu 8.01.2017.

Mawaziri hao walikuwa natarajia kupigwa hatua ambazo zinaweza kuwasafishia njia mawaziri wakuu wao kujiunga, katika ishara kwamba makubaliano mapana ambayo yanahusisha masuala kama utawala, mali na ardhi vinaweza kujadiliwa. Uingereza ni msimamizi wa zamani wa kikoloni nchini Cyprus, na sasa inaednesha vituo viwili vy akijeshi kisiwani hapo.

Matumaini ya juu zaidi

"Iwapo kuna utayarifu kwa pande zote kufukia suluhisho la pamoja kwa masuala yanayohusu ulinzi na usalama, ambayo upande wa Ugiriki unashiriki, basi waziri mkuu wa Ugiriki atasafiri kwenda Geneva na tutakuwa na uwezekano wa kutafuta suluhisho la haki na lenye kutekelezeka kuhusu suala la Cyprus," alisema Dimitris Tzanakopoulos, msemaji wa waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras.

Msemaji wa waziri mkuu wa Uturuki Binali Yildirim, alisema yeye pia alikuwa anasubiri ishara za maendeleo kutoka kw amawaziri w amambo ya nje. Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pia walikuwa wanashiriki katika mazungumzo hayo. Guterres alikuwa anatarajiwa kuzungumza na waandishi siku ya Alhamisi.

Uturuki ilipeleka wanajeshi karibu elfu 35 katika upande uliojitenga wa kaskazini mwaka 1974 baada ya kufanya uvamizi kufuatia mapinduzi yaliofanywa na Wacyprus wenye asili ya Ugiriki wakitumai kuiunganisha Cyprus na Ugiriki. Wacyprus wenye asili ya Uturuki ambao ndiyo wachache wanaiona nguvu ya kijeshi ya Uturuki kama uhakika wao pekee dhidi ya uhasama wa Wacyprus wa Uigiriki ikiwa makubaliano ya amani yatafumuka, na wanasisitiza juu ya kuyabakisha majeshi ya Uturuki kama sehemu ya makubaliano ya mwisho.

Schweiz Zyperngespräche in Genf (Reuters/P. Albouy)

Rais wa Cyprus ya Ugiriki Nicos Anastasiades akiwasili kwa ajili ya mazungumzo na mwenzake Mustafa Akinci.

Uwepo wa majeshi ya Uturuki

Wacyprus wagiriki wanachukulia uwepo wa majeshi ya Uturuki kama kitisho na zana ya ushawishi wa Ankara kisiwani hapo. Wanasisitiza kuwa Uturuki ambayo siyo mwanachama wa Umoja wa Ulaya, haipaswi kubakiza majeshi yake kisiwani hapo, wala kuwa na haki ya kuingilia kijeshi nchini Cyprus, ambayo ni sehemu ya kanda ya Umoja wa Ulaya.

Anastaciades na kiongozi wa Cyrpus ya Uturuki Mustafa Akinci wamekuwa wakiongoza mkututu wa mikutano migumu ya siri mjini Geneva tangu Jumatatu ili kutatua masuala kadhaa. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Cyprus Espen Barth, alisema Jumatano kwamba hatua zimepigwa kuhusu mambo kadhaa lakini kazi bado ni kubwa. Anastaciades na Akinci wote hawajuzungumza hadharani na waandishi kuhusu mazungumzo hayo tangu Jumatatu.

Mwandishi: Iddi Ssesanga/afpe,ape

Mhariri: Mohammed Khelef

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com