Mazishi ya mbunge wa upinzani Kenya yamepita kwa amani | Habari za Ulimwengu | DW | 09.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Mazishi ya mbunge wa upinzani Kenya yamepita kwa amani

Nairobi

Maelefu ya wakenya wameshiriki hii leo katika mazishi ya mbunge wa upande wa upinzani aliyeuliwa wiki iliyopita.Kisa cha kuuliwa David Kimutai Too kilizusha ghadhabu miongoni mwa wafuasi wa upande wa upinzani na kuzidisha wimbi la machafuko ya kikabila na mauwaji.Mazishi yake hii leo magharibi ya Kenya yamepita salama.Mazishi hayo yamefanyika siku moja baada ya serikali kuondowa marufuku ya mikutano ya hadhara,yaliyotangazwa baada ya uchaguzi wa december 27 iliyopita.Tangu wakati huo matumizi ya nguvu yaliyofuatia yamegharimu maisha ya zaidi ya watu elfu moja na wengine zaidi ya laki tatu na nusu kuyahama maskani yao.Katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi Annan yuko Nairobi akiongoza juhudi za amani kati ya serikali na upande wa upinzani nchini Kenya.Duru ya jana ya mazungumzo hayo ya amani imemalizika kwa matumaini mema huku mpatanishi wa Umoja wa Afrika Kofi Annan akielezea uwezekano wa kupatikana maridhiano mnamo siku chache zijazo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com