Mayweather na Pacquiao: Nani mkali? | Michezo | DW | 18.04.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Mayweather na Pacquiao: Nani mkali?

Ni pigano ambalo limesubiriwa na ulimwengu mzima. Mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wanapanda ulingoni katika kipindi cha wiki mbili zijazo. Lakini kufikia sasa bado tikiti za pigano hilo hazijaanza kuuzwa

Pigano hilo la Mei 2 mjini Las Vegas, Marekani, limekuwa likipangwa kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita, na sasa wakati wa kujigamba kwa maneno kati ya mabondia hao umekwisha.

Na hata wakati vigogo hao wakiendelea na mazoezi yao, bondia Mfilipino Pacquiao ameelezea matumaini kuwa Mmarekani Mayweather anayetumia sana mbinu ya kujikinga, mara hii ataonyesha mchezo mzuri wa kupambana ndani ya ulingo.

Mapema wiki hii, Mayweathwer alimtaja Pacquiao kuwa ni “bondia anayepigana kiholela bila uangalifu” na anayejiweka katika hatari ya kurushiwa makonde, na wakati Pacquiao akiwa na furaha kukubaliana na tathmini hiyo, pia anaamini kuwa mazoezi anayoyafanya kwa sasa yatamweka katika hali nzuri tayari kwa pigano hilo kubwa kabisa.

Mayweather mwenye umri wa miaka 37 ana rekodi nzuri kabisa ya kushiriki mapigano 47 bila kushindwa lolote akiwa na ushindi 26 aliopata kwa njia ya knockout. Pacquiao aliye na umri wa miaka 36, ameshiriki mapigano 57 na kushinda 38 kwa njia ya knockout. Hivyo sisi ni kuhesabu tu siku zilizosalia na kisha kuangalia jinsi mambo yatakavyokwenda ulingoni..

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com