1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mayweather na Pacquiao kupatana ulingoni

7 Machi 2015

Mashabiki wengi wa masumbwi wanalisubiri kwa hamu na ghamu pigano Kati ya bondia Mmarekani Floyd Mayweather Jnr na Mfilipino Manny Pacquiao. Wengi wanasema litakuwa pigano kubwa katika historia ya sasa

https://p.dw.com/p/1Emyt
Bildergalerie Sport Highlights 2012
Picha: AFP/Getty Images

Kocha au mkufunzi wandondi Freddie Roach ambaye Alhamisi wiki hii alitimiza umri wa miaka 55, amesema amejionea mengi akiwa kandoni mwa mabondia maarufu duniani, lakini kuwa mkufunzi wa Manny Pacquiao kwa pambano la kukata na shoka dhidi ya Floyd Mayweather bingwa wa uzito wa welter na ambaye hakushindwa hata pambano moja kati ya 47 hadi sasa itakuwa changamoto kubwa kabisa katika maiha yake.

Roach amewafunza mabingwa kadhaa kama Bernhard Hopkins, Julio Cesar Chavez na Oscar De la Hoya na amekuwa na Mfilipino Pacquiao kwa miaka 15, akichaguliwa kocha bora wa mwaka wa ndondi Marekani mara saba .

Alimtaja Mayweather kuwa asiyeshindika, mwenye maarifa na kipaji na bondia wa aina ya pekee, lakini ushindi wa Pacquiao watakapozipiga mjini Las Vegas , Mei 2 utamaliza yote hayo.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman
Mhariri:Josephat Charo