1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mayweather apokonywa taji aliloshinda dhidi ya Pacquiao

8 Julai 2015

Bingwa wa dunia wa uzani wa Welter Mmarekani Floyd Mayweather amepokonywa ukanda alioutwaa baada ya kumchapa Mfilipino Manny Pacquiao mwezi Mei. Mayweather anaruhusiwa kukata rufaa

https://p.dw.com/p/1Fupl
Floyd Mayweather Jr. celebrates the unanimous decision victory during the welterweight unification championship bout
Picha: Getty Images

Mayweather mwenye umri wa miaka 38 alishidnwa kulilipa shirikisho la ndondi duniani la WBO ada ya dola za Kimarekani laki mbili kabla ya kukamilika muda wa mwisho wa Julai 3.

Mayweather alitakiwa pia kutoa ukanda wa chipukizi wa WBO punde baada ya kumshinda mfilipino Pacquiao kwa wingi wa alama.

Kufuatia kauli hiyo ya shirikisho la ndondi la WBO, Mayweather hatambuliwi tena kama bondia anayeshikilia taji hilo kwa sasa. Taji hilo linashikiliwa na Mmarekani mwenza Timothy Bradley.

Mayweather alikuwa ameiahidi WBO kuwa akimshinda Pacquiao, angevua mataji yote ya vijana ili kuwapa mabondia wapya fursa ya kuwania mataji hayo lakini hadi kufikia sasa hajafanya hivyo.

Mayweather anatarajiwa kuandaa pigano lingine mjini Las Vegas tarehe 12 Septemba, japo haijabainika atazichapa dhidi ya nani.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Caro Robi