Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Kimataifa wamaliza mazungumzo mjini Goma | Matukio ya Afrika | DW | 17.09.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Kimataifa wamaliza mazungumzo mjini Goma

Kikao cha mawaziri wa ulinzi toka jumuiya ya kimataifa kwa ajili ya kanda ya maziwa makuu kimekamilishwa mjini Goma.

Ramani ya Kongo

Ramani ya Kongo

Kikao hicho kikiwa kinafuatia mazungumzo ya marais wa jumuiya hiyo kilichofanyika Kampala Uganda mapema mwezi huu,kilikuwa na lengo ya kubuni tume ya maofisa wa ujasusi ishirini na wawili, watakao chunguza hali ya mambo kwenye mipaka baina ya DRC na Rwanda,DRC na Burundi na pia DRC na Uganda. Na kikiwa kinasubiriwa Congo kikosi huru kwa ajili ya kuwafyeka waasi, waziri wa ulinzi wa Uganda akiwa ndie mwenyekiti wa kamati ya mawaziri wa ulinzi toka kanda hiyo anadhani kwamba, vita katika DRC vinaweza kumalizika pia kwa kupitia mazungumzo. John Kanyunyu na ripoti kamili kutoka Goma.

(Kusikiliza ripoti bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: John Kanyunyu

Mhariri:Mohammed AbdulRahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada