Mawakili walalamika kutoruhusiwa kumuona Ilunga | Matukio ya Afrika | DW | 16.09.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Mawakili walalamika kutoruhusiwa kumuona Ilunga

Mawakili wa aliyekuwa waziri wa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Oly Ilunga, wamelalamikia hatua ya kutoruhusiwa kukutana na mteja wao

Ilunga alikamtwa Jumamosi na kuwekwa rumande akituhumiwa kujaribu kutoroka kwenda nje ya nchi wakati uchunguzi ukuiendelea dhidi yake, kuhusiana na matumizi mabaya ya dola milioni 4,4 za kupambana na Ebola mashariki mwa Kongo

Polisi walizuwia mawakili hao kukutana na mteja wao, hapo jana kwa kile walichoeleza kuwa ni amri ya viongozi wa mahakama. Hatua hiyo ililalamikiwa na  Guy Kabeya, kiongozi wa bodi ya mawakili wa Oly Ilunga

akisema waliambiwa na polisi kwamba hawana haki ya kukutana na mteja wao. Kibeya amesema alipotaka maelezo zaidi,  afisa mwengine wa polisi alimwambia kwamba mawakili wamepigwa marufuku kukutana na Dr Oly Ilunga. K

Hata hivyo taarifa ya polisi imeeleza kwamba baada ya kuhojiwa na mwendesha mashataka, Ilunga alipigwa marufuku kutosafiri kwenda nje ya nchi. Lakini Polisi wamesema kwamba toka wiki kadhaa sasa, hawakufahamau mahali alipokuwa akiishi, na walimkamata huku akijaribu kuenda jimbo la Kongo-Central ili kuvuka mpaka wa Congo-Brazzaville.

Taarifa hiyo imetupiliwa mbali na mawakili wa Oly Ilunga ambao wamesema kwamba mteja wao,alikamatwa akiwa nyumbani kwake.

Oly Ilunga ambaye alikuwa waziri wa afya, amehojiwa na mwendesha mashataka kuhusu matumizi ya dola milioni 4.4 za serikali zilizotolewa kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Ebola.  Waziri huyo wa zamani ametuhumiwa kutumia vibaya fedha hizo, huku msaidizi wake na dereva wake pia wakiwa bado wanashikiliwa na polisi toka mwishoni mwa mwezi wa Agosti kwa sababu za uchunguzi.

Toka kujiuzulu kwake mwezi Julai, Ilunga alielezea kwamba amepata vitisho na shinikizo kutoka kwa watu ambao hakuwataja. Familia yake inaelezea kwamba  ameandamwa kutokana na hatua yake ya kujiunga na rais mstaafu Joseph Kabila mwishoni mwa mwaka 2016.

Oly Ilunga ambaye alikuwa Daktari binafsi wa Etienne Tshisekedi baba wa rais wa sasa Felix Tshisekedi, alikihama chama chake cha UDPS na kujiunga na serikali ya rais wa wakati huo Joseph Kabila.

Alipochaguliwa kuwa Rais, Felix Tshisekedi hakuwa na uhusiano mzuri na Waziri wake wa afya wakati ambapo ugonjwa wa Ebola umetapakaa katika majimbo ya Kivu ya kasazini na Ituri, hali ambayo iliathiri juhudi za kupambana na ugonjwa huo. Polisi inaelezea kwamba Oly Ilunga atafikishwa leo mbele ya mahakama kuu ya taifa ambako kesi yake itafunguliwa .