Mauaji yaitikisa Marekani | Matukio ya Kisiasa | DW | 10.07.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mauaji yaitikisa Marekani

Rais Obama atafupisha ziara yake katika mataifa ya kigeni na kwenda Dallas wiki ijayo wakati mashambulizi ya risasi yaliyofanywa na kijana mweusi ambaye ni mwanajeshi wa zamani aliyetia nia ya kuwauwa polisi wazungu.

NATO Gipfel in Warschau Obama PK zu Dallas

Rais Barack Obama wa Marekani

Mauaji hayo yamesababisha miito ya haraka kuleta hali ya kuvumiliana nchini humo kutokana na matatizo ya kibaguzi.

Polisi waligundua vifaa vya kutengenezea mabomu na silaha katika nyumba ya kijana huyo Micah Johnson mwenye umri wa miaka 25, mkaazi wa eneo la Dallas ambaye aliwapiga risasi polisi watano kabla ya kufariki katika mapambano ya silaha na polisi.

USA Ermordung von Polizisten in Dallas Täter Micah Xavier Johnson

Micah Xavier Johnson aliyewauwa polisi watano mjini Dallas

Ikulu ya Marekani ya White House imeondoa uwezekano wa mahusiano kati ya mshambuliaji huyo mwenye silaha na makundi yanayotambulika ya kigaidi, mahusiano katika ukurasa wake wa Facebook yanaelekeza katika makundi ya wanaharakati wenye msimamo mkali ya Wamarekani weusi ambayo yameorodheshwa kuwa ni makundi ya chuki nchini Marekani.

Akielezewa na polisi kuwa ni mshambuliaji aliyeamua kutenda kitendo hicho peke yake na hakuwa na rekodi ya uhalifu hapo nyuma , Johnson aliwaambia watu waliokuwa wanafanya nae majadiliano kabla ya kufariki kwamba alitaka kuwauwa polisi wazungu kwa kulipiza kisasi kutokana na kuuwawa kinyama hivi karibuni kwa watu wawili weusi.

USA Trauer nach Ermordung von Polizisten in Dallas

maua yakiwekwa katika eneo polisi walipouwawa mjini Dallas

Maandamano ya amani

Mashambulizi hayo jimboni Texas, ambayo yalizuka siku ya Alhamis usiku wakati wa maandamano ya amani dhidi ya ukatili wa polisi, yanakuja katika wakati wa hali ya kutafakari kuhusiana na matumizi ya silaha kwa ulinzi wa amani kuelekea Wamarekani weusi.

Viongozi wa harakati za Maisha ya Weusi ni muhimu wameshutumu mauaji hayo mjini Dallas, huku wakiapa kuendelea na maandamano yaliyopangwa kufanyika mwishoni mwa juma, huku makundi makubwa ya watu wakijikusanya usiku wa Ijumaa mjini Atlanta Georgia na wengine wengi wakiwa nje ya Ikulu ya Marekani White House.

Akihutubia maelfu ya watu katika sala iliyofanyika kwa heshima ya maafisa wa polisi waliouwawa, meya wa Dallas Mike Raswlings amewataka Wamarekani , kuimarisha hatua , kuponesha vidonda vya ubaguzi nchini humo.

USA Ermittlung nach Ermordung von Polizisten in Dallas

Magari ya polisi yakizuwia barabara kulinda usalama mjini Dallas

Maandamano yataendelea

"Hatutajitenga na ukweli uliopo kwamba sisi kama wakaazi wa mji, wa jimbo, na kama taifa tunapambana na masuala ya kibaguzi," ameliambia kundi la watu waliokusanyika.

Rawlings amerudia ujumbe uliotolewa na rais Obama wakati taifa hilo linahangaika kutokana na ghasia hizo za hivi karibuni: Kwamba maisha ya weusi ni muhimu , na kama ilivyo kwa maisha ya wazungu, wale maafisa wa polisi.

USA Trauer nach Ermordung von Polizisten in Dallas

Waombolezaji wakiweka maua katika eneo la mauaji

"Tunapaswa kuongeza nguvu na kuyakabili masuala tata kwa njia nyingine," amesema Rawlings. "Na masuala ya kibaguzi yanautata."

Obama , ambaye ameamuru bendera zote zipepee nusu mlingoti katika majengo ya serikali kwa muda wa siku tano, aliweka wazi kwamba ghasia dhidi ya polisi, haziwezi kuhalalishwa kabisa."

Rais alizungumzia mashambulizi hayo akiwa katika mji mkuu wa Poland, Warsaw , ambako alikuwa akihudhuria mkutano wa kilele wa NATO, na kuiita hali hiyo , "inayojirudia na ya kukera."

USA Dallas Schießerei bei Demonstrationen gegen Polizeigewalt

Polisi wakimtafuta muuaji

Ikulu ya Marekani imesema Obama atarejea nchini Marekani usiku ya Jumapili, siku moja kabla ya muda wake wa safari kumalizika, na kwenda kuzuru Dallas mapema wiki ijayo kwa mwaliko wa meya Rawlings.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Isaac Gamba

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com