1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauaji katika shule moja kusini mwa Ujerumani.

Munira Mohammad11 Machi 2009

Mwanafunzi mmoja mwenye umri wa miaka 17 amewafyatulia risasi wanafunzi na waalimu katika shule ya sekondari ya Albertville huko Winnenden karibu na Stuttgart.

https://p.dw.com/p/H9zv
Shule ya AlbertvillePicha: AP


Kansala wa Ujerumani, Angela Merkel, ametuma risala za rambirambi kwa jamaa ya wanafunzi na waalimu waliouawa katika shambulio lililotokea kwenye shule moja katika mji wa Sttutgart. Merkel alisema ni siku ya maombolezi kwa nchi nzima ya Ujerumani. watu 16 waliuawa, baada ya mshambuliaji mmoja aliyetambulika kama Tim K, kuwafyatulia risasi watu shuleni humo. Idadi hiyo ni pamoja na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 17, wanafunzi 9, waalimu watatu na wapita njia watatu. Mshambuliaji huyo aliyekuwa kajifunika uso wakati alipotekeleza mauaji hayo anasemekana aliwahi kuwa mwanafunzi wa shule hiyo shule hiyo ya Winnenden karibu na mji wa kusini mashariki mwa Ujerumani wa Stuttgart.



Ni tukio linaloendelea kuwashtua wengi, hasa kwa kuwa chanzo cha tendo hili la kinyama bado ni kitendawili. Wanafunzi wa shule ya mfumo wa pili ya sekondari ya Winnenden, karibu na mji wa kusini mwa Ujerumani wa Sttutgart, bado wapo katika mshtuko.


Taarifa zinasema mshambuliaji aliekuwa amevaa nguo nyeusi ....aliingia katika shule hiyo ya sekondari ya Albertville kiasi cha saa tatu na nusu asubuhi na kuanza kufyatua risasi katika kila upande... hakumsaza yeyote....alipomaliza watu 15 ikiwemo wanafunzi 9, waalimu 3 na wapita njia watatu......walikuwa wameuawa.



Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, katika taarifa yake alisema, '' ni siku ya majonzi na maombolezi kote Ujerumani, rambirambi zangu ziwaendee jamaa ya wanafunzi, waalimu na wote waliouawa, tupo pamoja nanyi katika msiba huu.''


Baada ya kutekeleza uovu wake, mshukiwa anasemekana alitoroka kwa gari alilokuwa ameliteka nyara....lakaini hakufika mbali...kilomita 40 tu naye akakutana na mauti yake....kupitia ufyatulianaji risasi na polisi.


Polisi tayari wameshika doria, helikopta za polisi zinapaa juu ya shule hiyo iliyo na wanafunzi wa kati ya umri wa miaka 10 na 16. Kituo cha biashara cha Winnenden, kilomita 25 kusini mashariki mwa mji wa Stuttgart, pia kimo chini ya ulinzi mkali.


Tukio hili, hapa Ujerumani lilitokea, saa kadhaa baada ya wenyeji wa jimbo la Alabama nchini Marekani kuamkia mshtuko baada ya mshambuliaji mwingine pia kuwaua watu 11 kwa kuwafyatulia risasi.


Kisa cha leo pia kinaleta ile kumbukumbu ya shambulizi baya kabisa kuwahi kutokea nchini Ujerumani mwaka 2002. Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 19, aliwaua kwa kuwafyatulia risasi, waalimu 12, wanafunzi 2, na polisi mmoja kabla ya kujiua mwenyewe.


'' Tumeshtushwa kabisa na mauaji haya, ndio ilikuwa sauti ya serikali ya Ujerumani.


Serikali ya Ujerumani ina sheria kali kuhusiana na matumizi na umiliki wa silaha.