Matumizi ya nguvu yazidi makali Jamhuri ya Afrika Kati | Matukio ya Afrika | DW | 30.05.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Matumizi ya nguvu yazidi makali Jamhuri ya Afrika Kati

Hali inatisha katika mji mkuu wa jamhuri ya Afrika Kati-Bangui ambako vizuwizi vimewekwa majiani na mapigano kuripotiwa kati ya vijana na vikosi vya polisi huku maelfu wakiandamana kudai serikali ya mpito ijiuzulu.

Wananchi wanafuatilizia hali namna ilivyo nchini mwao kupitia Radio,mfano wa bibi huyu

Wananchi wanafuatilizia hali namna ilivyo nchini mwao kupitia Radio,mfano wa bibi huyu

Mizinga kadhaa imefyetuliwa katika eneo la kati la mji mkuu wa jamhuri ya Afrika Kati -Bangui,karibu na kasri la rais katika wakati ambapo makundi ya waandamanaji waliongozana majiani.Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa AFP,hali ilitulia kidogo saa moja baadae baada ya waandamanaji kulihama eneo hilo.

Katika mitaa mengine na hasa karibu na uwanja wa ndege,mikururo ya watu wanaandamana wakidai serikali ya mpito ijiuzulu,wanajeshi wa kigeni waihame nchi hiyo na hasa wale wa kutoka Burundi wanaotuhumiwa kuwachia matumizi ya nguvu dhidi ya waumini wa dini ya kikristo.Watu wawili wanasemekana wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mapigano kati ya waandamanaji na vikosi vya kulinda amani vya kutoka nchi za Afrika Misca mjini Bangui.

Mji mkuu Bangui umejiinamia

Zentralafrikanische Republik Verletzte und Tote bei Zusammenstößen in Bangui 28.05.2014

Vifo na Majeruhi kufuatia mapigano mjini Bangui

Vikosi vya jeshi na polisi vimefyetua risasi hewani kuwatawanya waandamanaji.Vizuwizi vimewekwa majiani katika mitaa kadhaa ya mji mkuu.Hakuna magari yanayozunguka na,maduka yamefungwa.Mji mkuu mkuu huo umejiinamia helikopta ya kijeshi ya Ufaransa tu ndio inayopiga doria.Vikosi vya Ufaransa Sangaris na vile vya Misca vya kutoka nchi za Afrika vimeonya "vitapambana kikamilifu na aina yoyote ya mapendeleo".Vikosi hivyo vimetoa wito waa utulivu mjini Banguii.

Matumizi ya nguvu yamepamba moto tangu siku kadhaa sasa katika mji mkuu huo wa jamhuri ya Afrika Kati.Vizuwizi kadhaa viliwekwa katika njia muhimu na mapigano kuzuka kati ya vijana na vikosi vya nchi za Afrika kufuatia shambulio la kanisani lililoangamiza maisha ya watu wasiopungua 15.

Waziri mkuu André Nzapayéké anasema kuzidi nguvu machafuko "ni njama iliyoandaliwa" na "wanasiasa walio karibu na serikali."

"Kuna baadhi ya wanasiasa wanaoingia majiani wakidai serikali ijiuzulu,watu walio karibu na serikali,na karibu na rais wa mpito na baraza la mawaziri"Anasema waziri mkuu huyo.

Miito ya walimwengu dhidi ya matumizi ya nguvu

EU Afrika Gipfel in Brüssel 02.04.2014

Rais wa mpito Sanba -Panza na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon wakihudhuria mkutano wa kilele Kati ya Umoja wa ulaya na Afrika,mapema mwezi uliopita wa April

Umoja wa Ulaya unasema umeingiwa na wasi wasi wasi kutokana na hali namna ilivyo na kuwataka viongozi waendeleze bila ya kuchoka juhudi za kuleta suluhu ya taifa.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban ki-Moon amelaani vikali mashambulio yanayoendelea ikiwa ni pamoja na lile dhidi ya kanisa kuu la Fatima mjini Bangui.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AFP/Reuters

Mhariri:Yusuf Saumu