1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake magazetini

Oumilkheir Hamidou
21 Novemba 2018

Matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake majumbani, kudhoofika vyama vikuu nchini Ujerumani na kupigwa marufuku magari yanayotumia dizeli katika mji wa Hamburg ni miongoni mwa mada magazetini.

https://p.dw.com/p/38dtP
Häusliche Gewalt gegen Frauen Symbolfoto
Picha: picture-alliance/empics/D. Lipinski

Tunaanzia na ripoti za kutisha za matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake majumbani mwao. Gazeti la "Hannoversche Allgemeine" linaandika: Matumizi ya nguvu majumbani na visa vya kutumiliwa nguvu wanawake si jambo ambalo ni nadra kutokea. Takriban wahanga 140,000 wanajulikana, na 116,000 wanatuhumiwa kuhusika na visa hivyo. Katika daraja ya shirikisho  suala hilo angalao hivi sasa linashughulikiwa. Hata hivyo  watu hawapaswi kunyamaza na kuwakodolea macho wanasiasa.

Matumizi ya nguvu naiwe majumbani au njiani si sana kufanyika bila ya mashahidi. Ni sawa kabisa, si rahisi kuingilia kati ikiwa  katika nyumba ya jirani mke na mume wanakaripiana au mwenzako anakuja kazini akijaribu kuficha majeraha mwilini. Ni muhimu kutofumba macho. Kila mmoja anaweza kuuliza masuala na ikilazimika kuwapigia simu polisi. Asiyefanya chochote anachangia kuzidisha balaa hilo."

Vyama vikuu vitapa tapa nchini Ujerumani

Vyama vikuu nchini Ujerumani Social Demorat SPD na Christian Democratic CDU vinatangatanga kutokana na kishindo cha kuzidi kupoteza imani ya wapiga kura. Gazeti la "Mittelbayerische Zeitung" linachambua haki namna ilivyo katika chama cha CDU na kuandika: "Chama kilichokuwa zamani kikisifiwa kuwa ni chama kikuu kilipata pigo kubwa katika chaguzi zilizopita, kwa namna ambayo hautapita muda mrefu kinaweza kukabiliwa na hatari ya kupoteza madaraka yake katika serikali kuu mjini Berlin. Hali mpya ya kisiasa imeibua nguvu mpya. Katika chama cha CDU watu wanajadiliana, wanazozana na kupima na kutafakari. Matokeo yake ni kwamba kuna watakaopata imani ya wanachama na wengine watakao ondoka patupu. Kama hali namna inavyokuwa katika maisha ya kawaida."

Magari ya dizeli kuzuwilia kupita katika baadhi ya miji

Wenye magari yanayotumia dizeli nchini Ujerumani hawana tena raha. Mabadiliko ya tabianchi yamesababisha hatua kadhaa kuchukuliwa katika daraja za mikoa , kupiga mjarufuku magari kama hayo kupita katika miji kadhaa. Katika mji huu wa Bonn na pia katika mji wa Cologne, magari hayo hayarauhisiwi kupita katika maeneo ya kati  ya miji hiyo kuanzia April mwakani.Gazeti la "Flensburger Tageblatt" linazungumzia kuhusu marufuku kama hayo katika mji wa kaskazini wa Hamburg na kuandika: Mji wa Hamburg ulikuwa wa mwanzo kati ya miji ya Ujerumanim kupiga marufuku magari ya zamani yanayotumia dizeli yasipite katika barabara za mji huo.

 Matokeo ya uamuzi huo yameshachapishwa: Marufuku ya magari ya dizeli kupita katika eneo dogo lililotengwa hayakusaidia kupunguza moshi wa sumu kama ilivyokuwa ikitarajiwa. Kinyume chake ndicho kilichoshuhudiwa. Ikiwa vipimo vya miezi iliyopita vitathibitisha kuwa ni sawa na vya mwaka mzima, basi marufuku ya magari ya dizeli yatakuwa na athari kubwa zaidi ya faida. Na hili halimshangazi yeyote. Moshi wa sumu unaotoka ndani ya magari na viwandani haujali marufuku, unatapakaa tu majiani .

 

Mwandishi:Hamidou Oumilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Iddi Ssessanga