1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo yakoje Geita ambayo ni ngome ya Rais Magufuli?

29 Oktoba 2020

Katika kanda ya Ziwa Victoria nchini Tanzania mchuano mkali ni kati ya Vyama vya CCM na Chadema. Hiyo ni kanda inayoaminika kuwa ni ngome ya Mgombea wa rais kupitia CCM John Magufuli ambaye anatoka mkoa wa Geita.

https://p.dw.com/p/3kayl
Tansania | Präsidentschaftswahlen | Queen Sendiga
Picha: Ericky Boniphace/DW

Siku ya kwanza baada ya watanzania kukamilisha zoezi la kupiga kura kuchagua wabunge,madiwani na Rais,mkoani Mwanza malalamiko juu ya Rafu kwenye Uchaguzi yanaibuka siku moja baada ya kupiga Kura.

Sauti za wananchi wakiongozwa na mgombea Ubunge wa Jimbo la Nyamagana John Pambalu baada ya kumkamata mtu ambaye alikuwa anaingia kwenye kituo cha kupigia kura akiwa na karatasi zinazohusishwa na karatasi za kura.

Kambi ya Upinzani katika majimbo ya ukanda wa ziwa imelalamika mawakala wake kuondolewa kwenye vituo vya kupigia kura pamoja na kuwa walipata viapo, mawakala wa Chama cha ACT Wazalendo walijikuta wakizuiliwa kuingia kwenye vituo katika jimbo la Ukerewe na kusababisha malalamiko kutoka ACT.

Ukimya umetawala maeneo mengi katika ukanda wa ziwa wakati maeneo hayo yakisubiri kupata matokeo ya mwisho.

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea katika majimbo ya Ukanda wa Ziwa ambapo Chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema kimelipoteza kimepoteza ngome yake ya kwanza katika ukanda wa Ziwa baada ya Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Tarime vijijini kumtangaza Mwita Mwikabe Waitara kuwa mshindi wa nafasi ya Ubunge.

Mpiga kura kituoni Dar es Salaam
Mpiga kura kituoni Dar es SalaamPicha: Ericky Boniphace/DW

Waitara amemuangusha mshindani wake mkuu John Heche kutoka Chama cha Chadema huku jimbo la Tarime Mjini, aliyekuwa anatetea jimbo hilo Ester Matiko wa Chama cha CHADEMA akiangushwa na  Michael Mwita Kambaki CCM.

Katika mkoa wa Mwanza, wengi wanayamulika majimbo ya Nyamagana,Ilemela, Buchosa na Ukerewe ambapo wakati wa kampeni,mchuano mkali ulikuwa ni kati ya CCM na Chadema,mpaka hii sasa bado matokeo katika majimbo ya mkoa wa Mwanza yalikuwa hayajatangazwa huku mchuamo mkali ukiwa ni kati ya anayetetea kiti Stanslaus Mabula wa CCM na John Pambalu wa Chadema.

Mkoa wa Geita unaotajwa kuwa ngome ya Chama tawala CCM,bado majina ya washindi hayajatangwa,mkoa wa Kagera umekuwa na ushindani kati ya CCM na Chadema huku majimbo ya  Bukoba Mjini na Kyerwa yakitazamwa na wengi kutokana na ushindani mkali kati ya CCM na Chadema. Baadhi ya wananchi wameelezea jinsi walivyoliona zoezi la kuuanzia kupiga kura mpaka sasa zikihesabiwa.

Hadi tukienda mitamboni bado matokeo katika majimbo mengi kanda wa ziwa hayajatangazwa,huku kura za Uraisi zikionekana kwenda kwa mgombea kupitia CCM,John MAGUFULI ambaye kwa kura za awali amewaacha mbali washindani wake wote katika ukanda wa ziwa victoria.