Matokeo ya uchaguzi wa Israel ? | Magazetini | DW | 11.02.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Matokeo ya uchaguzi wa Israel ?

Uchaguzi huo utakua na athari gani kwa amani ?

Livni na Netanyahu(bega kwa bega)

Livni na Netanyahu(bega kwa bega)

Safu za wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo zimechambua mada mbali mbali tangu za ndani hata za nje:Nje,juu ya matokeo ya uchaguzi wa Israel na athari zake,lakini pia juu ya mpango wa Rais Barack Obama wa kuustawisha uchumi wa Marekani.

"Wapigakura wa Israel hawakuvichagua vyama vya mremngo wa kulia kabisa kinyume na ilivyohofiwa. Ndio, Natanyahu mwenye siasa kali na chama chake cha LIKUD anaingia Kneset-Bungeni akiwa na nguvu zaidi,lakini chama cha KADIMA cha waziri wa nje Bibi Livni, kimetia fora.

Chama gani lakini mwishoe, kitatamba na kuongoza serikali, bado si wazi.Majadiliano yatakuwa marefu na ya mwendo wa konokono kutokana na vyama vingi vidogo-vidogo vilivyonyakua viti Bungeni.

Osnabrucker Zeitung linahisi kwamba Bibi Livni kimsingi, ana nafasi kwa ushirikiano na chama cha Leba cha waziri wa ulinzi Ehud Barack, kuunda serikali ya muungano.Kuifikia lakini shabayha hiyo laandika gazeti:

"Watahitaji mshirika ambae walishindwa kumpata miezi michache iliopita.Endapo mwisho Netanyahu atatamba na kuwapiku wao,kuna hatari wazi kwa utaratibu wa amani ukasimama kabisa."

likitubakisha katika mada hii,gazeti la Westdeutsche zeitung kutoka Dusseldorf laandika:

".........Rais barack Obama ana azma ya kuzungumza tangu na syria hata na Iran na kuupa nguvu mpya utaratibu wa amani baina ya Waisraeli na wapalestina.Kuifikia shabaha hiyo lakini hatakubali kutiwa munda si na Natanyahu wala Bw.Lieberman,kinyume chake.Kila serikali yenye siasa kali ya Israel ikijaribu kuzichafua juhudi za amani,ndipo Marekani itakapo vinjari zaidi kutumia nguvu zake na kuingilia kati moja kwa moja kuusogeza mbele utaratibu wa amani.Ni kiroja cha mambo,lakini Israel kuelemea mrengo wa kulia mno,mwisyhoe kunaweza kukaleta baraka zake endapo Rais Obama akichukua juhudi za kweli.Na hayo ameahidi kufanya."

likiuchambua mpango wa rais Obama wa kuustawisha uchumi wa Marekani kwa jicho la msukosuko wa sasa wa fedha,gazeti la Flensburgerblatt lauliza:

"Je,yote aliyosema Obama ni vitisho vya kisiasa ili aweze kutimiza mradi wake ?

Au ni kweli hali ya uchumi wa Marekani ni mbaya hivyo ? ukilinganisha na misukosuko ya zamani kuna jibu wazi:Katika nafasi milioni 3.6 za kazi zilizopotea,sehemu kubwa kabisa ilikua mnamo miezi 4 iliopita.Hali hii ni mpya na tofauti kuliko ya misukosuko ya nyuma.Kufumba mikono na kutotenda lolote,ni onyo la rais Obama kwa wapinzani wanaoupinga mradi wake.Nyuma ya mkakati huo, ni mtego wake kuja kulipiza kisasi wakati wa uchaguzi wa Bunge la Kongress hapo mwakani 2010.Na hii lakini, si dhamana kisiasa."