1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matarajio ya wanasiasa wa Ulaya katika uchaguzi wa Marekani

Sekione Kitojo
7 Novemba 2016

Fikiria uchaguzi wa Marekani na kisha Donald Trum ameshinda. Hilo linawatia hofu kubwa wanasiasa wa Ulaya, na kwamba Clinton anaonekana kuelewa zaidi uhusiano kati ya Ulaya na Marekani.

https://p.dw.com/p/2SI74
Kombibild Trump Clinton
Picha: picture alliance/abaca/O. Douliery/newscom/N. Redmond

Hebu  fikiria ,  kwamba  uchaguzi  unafanyika  nchini Marekani  kesho  Jumanne (08.11.2016) na  kisha  Trump  ameshinda. Bara  la  Ulaya  linahofu  kubwa  na  fikira  hiyo. Hillary Clinton  kinyume  chake  anaonekana  kueleweka  zaidi katika  uhusiano  kati ya  maeneo  haya  mawili yanayotenganishwa  na  bahari  ya  Atlantic.  Ni  nani  kwa mtazamo  wa   watu  wa  Ulaya  anafaa  kushinda uchaguzi  huu.  

Kuna  jengo  moja  peke  yake  katika  bara  la  Ulaya kijiongrafia , ambalo  lina  jina  la  Donald Trump. Jengo hilo  liko  mjini  Istanbul  nchini  Uturuki. Lakini   tangu mwaka  2015 , wakati  mgombea  wa  kiti  cha  urais  nchini Marekani  aliposema  anapinga  Waislamu  kuhamia  nchini Marekani , wanasiasa  wa  Uturuki  pia  wanataka  kufuta jina  la  Trump  katika  jengo  hilo.

Donald Trump
Donald Trump wa chama cha Republican Picha: Picture-Alliance/AP Photo/E. Vucci

Pamoja  na  hayo  kundi  la  makampuni  ya  Trump limejenga  viwanja  kadhaa  vya  mchezo  wa  golf  katika bara  la   Ulaya.  Na  hilo  ndio   jambo pekee    linaloleta uhusiano  kati  ya  Donald Trump  na  Ulaya.

Na  tangu Donald Trump  alipofanya  ziara  nchini Scotland  mwezi  Juni  mwaka  huu  si  jambo  la  kudai, lakini  aliiteka  na  kuwafanya  watu  wavutike  upande wake. Na  ndivyo  alivyofanya  hadi  kuteuliwa  kuwa mgombea  katika  uchaguzi  wa  Marekani.

Mbunge  wa  Ujerumani  katika  bunge  la  Ulaya , David MacAllister ambaye  naye  binafsi  ana  asili  ya  Scotland , amemueleza  mgombea  huyo  wa  chama  cha Republican kama  hivi:  "Donald  Trump  hatambuliki  sana kwetu  sisi  watu  wa  Ulaya. Hatufahamu  mengi  kumhusu yeye. Hatufahamu  mengi  kuhusiana  na  sera  zake  za mambo  ya  kigeni, kwa  kuwa  hazungumzi  mengi  kuhusu hilo.

USA | 3. Präsidentschaftsdebatte 2016 in Las Vegas
Mgombea wa chama cha Democratic Hillary ClintonPicha: picture-alliance/AP Photo/P. Semansky

Na  iwapo  utaingia  kwa  undani  zaidi , inaleta  kidogo hofu. MacAllister  ni  mwenyekiti  wa  kundi  la  bunge  la Ulaya , ambalo  linashughulika  na  masuala  ya  uhusiano kati  ya  Ulaya  na  Marekani.

Ni  wazi  kwamba  tunamfahamu  Hillary Clinton  vizuri zaidi  hapa  Ulaya. Anaamini  kuhusu  uhusiano  imara  kati ya  Ulaya  na  Marekani. Pamoja  nae  tunahakika  ya kufanikisha  mambo  mengi.  Kwa  kuwa  waziri  wa  zamani wa  mambo  ya  kigeni  Hillary Clinton amekutana  na wanasiasa  wengi   wa  Ulaya  waliopo  hivi  sasa.

Uhusiano na  Ulaya

Kwa  hiyo  mtu  anatarajia  hali  ya  muendelezo  wa mambo.  Hadi  sasa  maraisi  wengi  kutoka  chama  cha Democratic  na  Republican  waliendeleza   hali  ya  uimara wa  jumuiya  ya  NATO. Lakini  Donald Trump  tayari ameitikisa   jumuiya  hiyo  ya  ulinzi  katika  mataifa  hayo ya  Atlantic.  Anataka  tu  kuendelea  na  jumuiya  hiyo pale Ujerumani  itakapolipia  usalama  wake.

David McAllister  anajaribu  kuyaeleza  matarajio  yake  kwa njia  ya  kidiplomasia. Marekani  na  Umoja  wa  Ulaya wana  uhusiano  wa  karibu  sana . Tunapaswa  kuweka mtazamo  wetu  katika  kuimarisha  hali  hii, bila  kujali matokeo  ya  uchaguzi. Tunapaswa  kujitayarisha  kwa  hali mbaya  ama  nzuri.

Republik Moldau Europa-Symposium David McAllister Universität Chisinau
Mbunge wa Ujerumani katika bunge la Ulaya David McAllisterPicha: ppe.md

Kuna  wapenzi  wa  Trump  lakini  hata  katika  makao makuu  ya  Umoja  wa  Ulaya, hususan  wanasiasa  wa mrengo  wa  kulia. Mbunge  wa  Uingereza  katika   bunge la  Ulaya  Nigel  Farage  alishiriki  katika  mkutano  wa kampeni  ya  uchaguzi  ya  Donald Trump. Kutokana  na ukosoaji  mwingi  dhidi  ya  Trump  kuhusu  matamshi  yake na  vitendo  vya  kuwadhalilisha  wanawake , Farage alisema  wakati  alipohojiwa  na  kituo  cha  televisheni  cha Fox  nchini  Marekani  kwamba , Donald Trump  ni binadamu, na  kila  binadamu  ana  doa  lake, ambalo  kwa Trump  tunalijua  lakini  hatujui  lolote  la  siri  kwa  upande wa  Clinton hadi  sasa.  Ameongeza  kwamba anachaguliwa  rais  wa  Marekani   na  sio  baba  mtakatifu.

Wolfgang Schäuble Bundesfinanzminister
Wolfgang Schäuble waziri wa fedha wa UjerumaniPicha: picture-alliance/AA

Waziri  wa  fedha  wa  Ujerumani  Wolfgang Schaeuble alisema  katika  mkutano   mjini  Luxemburg  alishangazwa sana  alipomsikia  Trump  katika  mdahalo  katika televisheni  akimtishia   Clinton  kwamba  atamkamata akichaguliwa  kuwa  rais.

Waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Ujerumani Frank-Walter Steinmeier  amemuita  Donald Trump  kuwa  ni  mhubiri  wa chuki.

Mwandishi: Bernd Riegert / ZR /  Sekione  Kitojo

Mhariri: Yusuf  , Saumu