Katika matangazo yetu leo mchana: Iran yafanya majaribio mapya ya kombora la masafa marefu. Wagombea katika uchaguzi mkuu wa Ujerumani watafuta kura za mwisho mwisho kabla ya uchaguzi wa hapo kesho. China yaishinikiza Korea Kaskazini kwa kutekeleza vikwazo dhidi ya nchi hiyo.