Mataifa sabaa tajiri kiviwanda yapania kuyaokoa masoko ya fedha | Habari za Ulimwengu | DW | 11.10.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mataifa sabaa tajiri kiviwanda yapania kuyaokoa masoko ya fedha

Mpango maalum wa kuzuwia balaa la kutapakaa mzozo wa fedha wabuniwa na mawaziri wa fedha wa G7 na wakuu wa benki mashuhuri za dunia mjini Washington

Washington:


Mataifa sabaa tajiri zaidi kiviwanda yanaandaa mpango wa vitendo wa kuepukana na balaa la kuenea mzozo wa fedha.Mawaziri wa fedha na wakuu wa benki kutoka mataifa sabaa tajiri zaidi kiviwanda wamekubaliana mjini Washington,kuhusu mpango huo wa vifungu vitano kwa lengo la kuzihifadhi benki kubwa kubwa zisifilisike na kutengwa fedha za serikali ili kugharimia mikopo.Waziri wa fedha wa serikali kuu ya Ujerumani Peer Steinbrück amezungumzia juu ya "ishara bayana" iliyotolewa.Amedokeza hata serikali kuu ya Ujerumani itachangia katika mpango huo wa kuzinusuru benki. Waziri mwenzake wa Marekani Henry Paulson amesema baada ya mkutano huo mjini Washington,viongozi wa Marekani wataanza hivi karibuni kununua hisa za benki zilizo hatarini.Mawaziri wa fedha na wakuu wa benki wamekutana mjini Washington baada ya mipango ya serikali tofauti ya kumimina mafedha  na kupunguza viwango vya riba kushindwa kutuliza hali ya mambo katika masoko ya hisa.

 • Tarehe 11.10.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FY4G
 • Tarehe 11.10.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FY4G
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com