Mataifa kadha yashutumu hatua za Musharraf. | Habari za Ulimwengu | DW | 04.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mataifa kadha yashutumu hatua za Musharraf.

Wakati huo huo jumuiya ya kimataifa imeshutumu kwa kiasi kikubwa hali nchini Pakistan . Nchini Marekani , msemaji wa Ikulu ya nchi hiyo amesema kuwa Musharraf anahitaji kutimiza ahadi zake kuendesha nchini humo uchaguzi huru na wa haki, wakati ambapo waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza David Miliband amesisitiza haja ya Pakistan kutumia uwezo wa demokrasia na utawala wa sheria.

India haikutoa taarifa kali ila imesema kuwa inasikitishwa na hatua hiyo. Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhuto , ambaye amerejea hivi karibuni nchini Pakistan baada ya miaka nane ya kuishi uhamishoni , ameahidi kuwa chama chake kitachukua hatua dhidi ya amri hiyo ya hali ya hatari akiita sheria ya kijeshi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com