1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa 90 yakiuka kwa kiasi kikubwa haki za kibadamu.

Jane Nyingi14 Januari 2009

Kenya, Burundi,Rwanda,Liberia na Uganda ni miongoni mwa mataifa 90 duniani ambayo yameripotiwa visa vingi vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

https://p.dw.com/p/GYNa
Watu wakikimbilia usalama punde baada ya kutokea machafuko kufuatia uchaguzi mkuu nchini Kenya 2007.Picha: AP

Hayo yamo katika ripoti ya mwaka huu ya Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadam Human Rights Watch.

Uchaguzi mkuu nchini Kenya uliokabiliwa na utata ndio umelifanya taifa hilo kuingia katika orodha hiyo. Zaidi ya watu elfu moja na mia tatu walipoteza maisha yao na zaidi ya laki tatu kuachwa bila makao.Utata huo uliyachochea makundi ya vijana kufanya machafuko na kundaa maandamano katika miji mbalimbali nchini Kenya.

Kwa mujibu wa ripoti ya tume ya waki, miongoni mwa tume zilizobuniwa kuchunguza utata uliozunguka uchaguzi huo mkuu polisi waliwaua kwa kuwapiga risasi zaidi ya watu 400.

Iliwabidi wapatanishi wa kimataifa kuingilia kati na kuzipatanisha pande zilizokuwa zinazozana kisiasa , na hapo serikali ya muungano wa kitaifa ikabuniwa nchini Kenya.Hata hivyo ilipendekeza kufanywa kwa mabadiliko katika mfumo mzima wa upigaji kura nchini Kenya na katika tume ya uchaguzi nchini humo.

Ripoti hiyo ya Human Rights Watch inaaema kuwa nchini Liberia hali ya usalama humo imezorota tangu mwaka jana huku visa vya wizi wa kimabavu, ubakaji na maandamano ya mara kwa mara yakiripotiwa.Japokuwa serikali ya rais Ellen Johnson Sirleaf imejitahidi katika kukabiliana na ufisadi na kubuni mfumo kwa kuheshimu haki za kibindamu,ni hatua chache zimechukuliwa katika kufanikisha maswala hayo.

Ama nchini Burundi ripoti ya shirika hilo la kimataifa ya haki za binaadamu inasema kuwa juhudi za kutatua mzozo kati ya serikali na kundi la waasi la Palipehutu-FNL nchini Burundi hazijafua dafu.

Nchini Rwanda ni kutokana na mauji ya halaiki yaliyotekelezwa miaka 14 iliyopita.Ripoti ya shirika hilo inasema kuwa hadi sasa ni hatua chache zilizopigwa katika kuhakikisha wahusika wanachukuliwa hatua zifaazo.

Kwa upande wa Uganda ripoti hiyo ya Human Rights Watch inasema kuwa mwaka jana serikali ya rais Yoweri Museveni na waasi wa Lords Resistance army-LRA walishindwa kukamiisha utiaji saini mkataba wa amani na hivyo kupelekea wananchi wa eneo kaskazini mwa nchi hiyo kuishi katika hali ya wasiwasi kutokana na kuendelea kuwepo kwa hali tete kwenye eneo hilo.