1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Masharika ya kibinadamu yataka haki kwa wakazi wa Mombasa

Tatu Karema
30 Machi 2020

Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Kenya yameitaka serikali kuwakuchukuliwa hatua za kisheria maafisa wa usalama waliowapiga na kuwajeruhia abiria 30 katika kivuko cha Feri na kusababisha vifo vya watu wawili.

https://p.dw.com/p/3aBPL
Kenia Mombasa Fähre
Picha: DW/E. Ponda

Mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za binadamu la Muhuri, Khelef Khalifa amemtaka kamishna wa kaunti ya Mombasa Gilbert Kitiyo kujiuzulu kwa kutoa amri ya maafisa wa usalama kuwapiga raia. Kulingana na Muhuri amri hiyo ndio iliyosababisha mkanyagano wa watu baada ya maafisa wa usalama kutumia magongo kutawanya umati wa abiria waliokuwa wanataka kuabiri feri huku wakifyatua mabomu ya kutoa machozi. 

Kulingana na mwenyekiti wa shirika la msalaba mwekundu kanda ya Pwani, Mahmoud Noor, waliapa huduma za matibabu abiria 30 waliojeruhiwa na mwanamke mmoja aliyezirai kwa mshtuko. Wanaume wawili waliokuwa katika hali mbya walifikishwa katika hospitali kuu ya ukanda wa pwani ya Makadara ambapo mmoja alifariki na mwengine kufariki katika kaunti ya Kwale. Abiria wanaotumia feri hiyo wamelalamika juu ya taratibu uanotumiwa hivi sasa katika kivuko hicho na kuwalaumu maafisa wa usalama kwa kutumia nguvu.

Idara ya usalama imejitetea kwa kueleza kuwa walilazimika kuchukua hatua baada ya baadhi ya abiria kukataa kupanga foleni na kuanza kuwarushia mawe. Utaratibu wa kupanda feri sasa umebadilishwa. Muda mwingi utakuwa ni abiria pekee wanaovuka na magari yatavuka kutoka saa tano asubuhi hadi saa tisa mchana lengo likiwa kupunguza msongamano wa watu kama njia moja ya abiria kuepuka kusambaa kwa virusi vya Korona.