Mashabiki wa Bundesliga kuingia viwanjani | Michezo | DW | 16.09.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Mashabiki wa Bundesliga kuingia viwanjani

Wanasiasa katika majimbo yote ya shirikisho la Ujerumani wamekubaliana kuwa na utaratibu sawa wa majaribio wa kuwarejesha mashabiki wa soka viwanjani

Fußball Bundesliga | Freundschaftsspiel Union Berlin - 1. FC Nürnberg | Mit Fans

Baadhi ya mashabiki wakitazama soka, huku wakiwa wanazingatia umbali ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.

Wanasiasa katika majimbo yote ya shirikisho la Ujerumani wamekubaliana kuwa na utaratibu sawa wa majaribio wa kuwarejesha mashabiki wa soka viwanjani pale ligi kuu ya soka ya Ujerumani-Bundesliga itakapoanza msimu mpya mwishoni mwa juma hili.

Kwa mujibu wa utaratibu ulioafikiwa viwanja vitaruhusu mashabiki kujaza asilimia 20 ya uwezo wake kwa kipindi cha wiki sita za mwanzo. Baada ya kipindi hicho mwishoni mwa Oktoba, mamlaka husika zitafanya tathmini ya majaribio hayo.

Fußball Borussia Dortmund | Erling Haaland

Erling Haaland, mmoja ya chipukizi wa BVB, aliyejibebea sifa katika msimu uliopita kutokana na umahiri wake

Mkuu wa shirikisho la soka la Ujerumani, DFB, Fritz Keller amesema amefurahishwa sana na uamuzi huo. Licha ya uamuzi huo wa nchi nzima, jimbo la kaskazini mwa Ujerumani la Schleswig-Holstein linajipanga kuruhusu mashabiki wa hadi asilimia 25 ya uwezo wa viwanja vyake. 

Maamuzi hayo yanakuja katika muda muafaka ambapo Bundesliga na ligi nyingine za Ujerumani zikijiandaa kuanza kutimua vumbi kwenye viwanja visivyo na mashabiki. Hata hivyo, bado haiko wazi iwapo vilabu vyote vya Bundesliga vitaweza kutekeleza hatua hiyo kwa wakati, wakati kipute cha Bundesliga kinapoanza Ijumaa wiki hii, ambapo mabingwa watetezi Bayern Munich wakifungua msimu kwa kukutana na Schalke 04. 

Hali kuhusiana na maambukizi ya virusi vya corona, itatathminiwa tena mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Soma Zaidi: Bundesliga huenda ikabaki bila mashabiki hadi 2021