Maridhiano yamefikiwa nchini Ukraine uchaguzi uitishwe September 30 ijayo | Habari za Ulimwengu | DW | 27.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Maridhiano yamefikiwa nchini Ukraine uchaguzi uitishwe September 30 ijayo

Kiew

Rais Viktor JUSCHENKO wa Ukraine na waziri mkuu wa nchi hiyo VIKTOR JANUKOWITSCH wamesitisha kinyang’anyiro cha kuania madaraka.Baada ya mazungumzo yaliyodumu usiku kucha mjini Kiew,viongozi hao wawili wamekubaliana kuitisha uchaguzi wa bunge kabla ya wakati.Viongozi hao wawili wamekubaliana uchaguzi huo wa bunge uitishwe September 30 ijayo.Kabla ya hapo,rais JUSCHENKO anaeelemea upande wa magharibi alitaka uchaguzi uitishwe haraka zaidi huku mpinzani wake,waziri mkuu JANUKOWITSCH anaeelemea zaidi upande wa Urusi akishikilia ukawilishwe.Inatarajiwa maridhiano hayo yatatuliza wasi wasi ulioenea tangu wiki iliyopita.Mzozo wa Ukraine umeripuka tangu mwezi uliopita pale rais Yuschenko alipoamua kulivunja bunge na kutangaza uchaguzi kabla ya wakati.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com