1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yawawekea vikwazo maafisa wa Korea Kaskazini

Grace Kabogo
13 Januari 2022

Marekani imewawekea vikwazo maafisa watano wa Korea Kaskazini baada ya hivi karibuni nchi hiyo kufanya jaribio la makombora ya masafa marefu.

https://p.dw.com/p/45Sct
Nordkorea | Raketentest
Picha: KCNA/KNS/AFP

Wizara ya Fedha ya Marekani imesema maafisa hao watano wamewekewa vikwazo kutokana na michango yao ya kununua vifaa na teknolojia inayotumika kwa mipango ya makombora ya Korea Kaskazini.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeamuru vikwazo dhidi ya raia mwengine wa Korea Kaskazini, mmoja wa Urusi na kampuni ya Urusi kwa msaada wao mpana katika shughuli za Korea Kaskazini za silaha za maangamizi.

Marekani imeichukua hatua hiyo saa chache tu baada ya Korea Kaskazini kusema kiongozi wake Kim Jong Un aliongoza jaribio lililofanikiwa la kombora la kasi kubwa siku ya Jumanne ambalo ilidai litaongeza pakubwa uwezo wa nchi hiyo kujilinda dhidi ya vita vya nyuklia.