1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yataka msaada zaidi wa kijeshi Afghanistan

12 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CaSR

WASHINGTON:

Waziri wa Ulinzi wa Marekani,Robert Gates amesema,nchi zingine katika Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa ya Magharibi-NATO,zinapaswa kuziba pengo katika ujumbe wa jumuiya hiyo nchini Afghanistan.Gates ameiarifu Kamati ya Kijeshi ya Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani, kuwa machafuko yameongezeka nchini Afghanistan tangu vikosi vinavyoongozwa na NATO kuchukua dhima ya kulinda usalama katika mwezi wa Oktoba mwaka 2006.

Mara kwa mara,Marekani imetoa mito kwa wanachama wengine katika jumuiya hiyo ya mataifa 26, kupeleka wanajeshi zaidi na walimu wa kutoa mafunzo kwa polisi na majeshi ya Afghanistan kwa sababu sehemu kubwa ya vikosi vya Marekani vinashughulika zaidi nchini Irak.