1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Marekani: Uhalifu wa kivita ulifanywa katika vita vya Tigray

Bruce Amani
21 Machi 2023

Marekani imehitimisha kuwa pande zote katika mzozo wa kivita uliodumu kwa miaka miwili ambao umeuharibu mkoa wa kaskazini mwa Ethiopia wa Tigray zilihusika katika uhalifu wa kivita.

https://p.dw.com/p/4OyM4
Äthiopien Addis Abeba | Menschen aus der Region Tigraya demonstrieren vor der US-Botschaft
Picha: Seyum Getu/DW

Akizungumza wakati akiwasilisha ripoti ya uchunguzi, Waziri wa Mambo ya Kigeni Antony Blinken amesema kuwa wale waliohusika lazima wawajibishwe.

Ripoti hiyo inaweka uzito kwa tuhuma za awali kuhusiana na uhalifu uliofanywa, na kutoa wito wa kufunguliwa mashitaka. Ripoti hiyo ya kila mwaka ya haki za binaadamu pia ilisema pande zote isipokuwa tu Jeshi la Ukombozi wa Watu wa Tigray - TPLF zilihusika na uhalifu dhidi ya ubinaadamu.

Soma pia: Blinken aiomba Ethiopia kuimarisha amani baada ya vita

Blinken amesema uhalifu huo ni pamoja na mauaji, ubakaji, na aina nyingine za ukatili wa kijinsia pamoja na mateso. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, vita hivyo inaaminika vilisababisha mamilioni ya wakimbizi wa ndani.