1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaonya wanamgambo wa Taliban huenda wakaimarisha hujuma zao

28 Juni 2008

-

https://p.dw.com/p/ESId

WASHINGTON

Marekani imeonya kwamba kundi la Taliban huenda likaongeza nguvu mashambulio yake mwaka huu.Katika ripoti iliyotolewa na wizara ya ulinzi juu ya usalama nchini Afghanstan Marekani imeonya kuwa wanamgambo wakitaliban huenda wakaendeleza mashambulio au hata kuongeza opresheni zao za kigaidi nchini humo.Mapema wiki hii kamanda wa kijeshi wa Marekani nchini Afghanstan alifahamisha kuwa mashambulio ya wanamgambo hao wakitaliban katika eneo la mashariki ya Afghanstan yameongezeka kwa asilimia 40 mwaka huu ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwaka jana.

Hali hii inajitokeza licha ya juhudi za wanajeshi wa kimataifa za kuwakamata na kuwaua viongozi wa kitaliban.Kwa upande mwingine maafisa nchini Afghanstan wamedai kwamba uasi unaongezeka kutokana na Taleban kuruhusiwa kujificha katika maeneo ya kikabila ya mpakani na Pakistan.