1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yajaribu kufufua Majadiliano ya Amani

16 Julai 2010

Mjumbe maalum wa Marekani katika Mashariki ya Kati, George Mitchell, amefungua duru ya sita ya majadiliano yasiyo ya ana kwa ana, kati ya Waisraeli na Wapalestina.

https://p.dw.com/p/ONfD
U.S. Middle East envoy George Mitchell waves to the press before his meeting with Palestinian President Mahmoud Abbas, not pictured, in the West Bank city of Ramallah, Saturday, May 8, 2010. Palestinian leaders on Saturday gave their backing for indirect peace talks with Israel, clearing the way for the Obama administration's first sustained on-the-ground Mideast peace effort. U.S. envoy George Mitchell will now shuttle between the Israeli and Palestinian leaders for up to four months to try to narrow the vast gaps on the terms of Palestinian statehood. (AP Photo/Majdi Mohammed
Mjumbe wa Marekani katika Mashariki ya Kati, George Mitchell.Picha: AP

Mjumbe huyo maalum wa Rais wa Marekani, katika Mashariki ya Kati, George Mitchell, ameanzisha duru mpya ya majadiliano hayo yasiyo ya ana kwa ana, kwa kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Jerusalem. Kesho Jumamosi,amepanga kukutana na Rais wa Mamlaka ya ndani ya Wapalestina, Mahmoud Abbas mjini Ramallah katika Ukingo wa Magharibi, kabla ya kuwa na kikao cha pili pamoja na Netanyahu siku ya Jumapili.

unserem KORR Nahost/Gaza/Israel: **Azu RCHIV** Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu speaks after a meeting with Canadian Prime Minister Stephen Harper in Ottawa, Canada, Monday May 31, 2010. (AP Photo/The Canadian Press, Adrian Wyld)
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.Picha: AP

Ni matumaini ya Mitchell kuwa ataweza kumshawishi Rais Mahmoud Abbas kufanya majadiliano ya ana kwa ana, kabla ya kumalizika kusitishwa kwa muda ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika majira ya mapukutiko. Lakini hadharani,Rais Abbas na mpatanishi wake mkuu Saeb Erekat wameendelea kutoa masharti ya kurejea katika majadiliano ya ana kwa ana.

Palestinian President Mahmoud Abbas gestures during a news conference with the German Chancellor Angela Merkel (not in the picture) in the Chancellery in Berlin, Germany, Monday, Feb. 1, 2010. (AP Photo/Gero Breloer)
Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Wapalestina, Mahmoud Abbas.Picha: AP

Israel isitishe kabisa ujenzi wa makaazi ya walowezi katika Ukingo wa Magharibi na Jerusalem ya Mashariki iliyokaliwa kwa mabavu; majadiliano yaanze pale yalipoishia wakati wa utawala wa waziri mkuu wa zamani wa Israel Ehud Olmert; na kwanza maendeleo ya maana yapatikane wakati wa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja, kuhusu masuala muhimu ya kujadiliwa hasa yale yanayohusika na mipaka na usalama.

Lakini juma lililopita, Netanyahu alipokuwa ziarani Washington aliashiria kuwa hana nia ya kurefusha ule muda wa miezi 10 wa kuahirishwa harakati za ujenzi wa makaazi zaidi ya Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi, unaomalizika Septemba 26.

Ni matumaini ya Marekani na Israel kuwa mazungumzo ya moja kwa moja yataweza kufanywa kabla ya tarehe hiyo, ili viongozi wote wawili wapate nafasi ya kupitisha maamuzi magumu.

Lakini chama cha Fatah cha Rais Mahmoud Abbas kimemuhimiza kiongozi wake kutoshiriki katika majadiliano yasiyo ya moja kwa moja. Kinasema, majadiliano yanayofanywa tangu mwezi wa Mei, kupitia mjumbe maalum wa Marekani, hayakuleta chochote hadi hivi sasa.

Mjumbe huyo wa Obama, hatazamiwi kufafanua mazungumzo yake hadharani sawa na ilivyokuwa wakati wa ziara zake za hapo awali katika Mashariki ya Kati.

Mwandishi: P.Martin/AFPEDPAE

Mhariri:Charo,Josephat