Marekani yaipeleka puta Uingereza | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 13.06.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Marekani yaipeleka puta Uingereza

Marekani imeiendesha mchakamchaka Uingereza katika michuano ya fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini, kwa kuilazimisha kutoka nayo sare ya bao 1-1

default

Mlinda mlango wa Uingereza Robert Green akishuhudia mpira ukiingia wavuni baada ya kushindwa kuudhibiti mkononi

Uingereza ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya nne tu ya mchezo kupitia kwa nahodha wake Steven Gerrad, lakini uzembe wa mlinda mlango wao Robert Green kulegeza mikono iliiruhusu Marekani kusawazisha bao hilo kufuatia kombora la Clint Dempse.

England - USA WM Weltmeisterschaft Flash-Galerie

Steven Gerrard akishangilia bao la kuongoza

Gerrad amekiri kuwa matokeo hayo yamewaweka katika nafasi ngumu ya kusonga mbele.

Kwa upande wake kiungo mwengine wa Uingereza Frank Lampard alimtetea mlinda mlango huyo akisema kila mchezaji hufanya kosa dimbani.

Hata hivyo washabiki nchini Uingereza wanaonekana kumnyooshea kidole kocha Fabio Kapelo kwa kucheza kamari kumpanga Green, langoni, badala ya mkongwe David James.

Kulikuwa na taarifa kuwa baadhi ya wachezaji waandamizi katika timu hiyo walitaka David James aanze, kwani ana uwezo wa kuwapanga mabeki.

Katika mechi nyingine, mmoja kati ya wawakilishi wa Afrika Nigeria walifungwa bao 1-0 na Argentina, huku Korea Kusini ikiwafunga Ugiriki mabao 2-0.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com