1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaipa msaada Kenya na Uganda

11 Machi 2008

Rais George W. Bush wa Marekani ametowa dola milioni 4.9 katika msaada wa dharura wa wakimbizi kwa Kenya na Uganda kutokana na mgogoro wa kisiasa mjini Nairobi.

https://p.dw.com/p/DMMb

WASHINGTON

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Gordon Johndroe amesema hapo jana kwamba rais ameruhusu wizara ya mambo ya nje kutumia hadi dola milioni 4.9 kutoka Mfuko wa Marekani wa Msaada wa Dharura wa Wakimbizi na Uhamiaji kwa ajili ya Kenya na Uganda.

Fedha hizo watapatiwa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya wakimbizi na mashirika mengine ya kimataifa na yale yasio ya kiserikali.

Johndroe amesema katika taarifa kwamba fedha hizo hususan zitatumika kwa mahitaji ya kibinaadamu ya wakimbizi wanaozidi kuongezeka, watu waliopotezewa makaazi yao ndani ya nchi na wahanga wa mizozo nchini Kenya na Uganda.