1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaionya Tanzania kuhusu mauaji

16 Februari 2018

Marekani kupitia ubalozi wake Dar es Salaam imeeleza kusikitishwa na kitendo cha utekaji nyara na vurugu zilizosabisha kifo cha kada wa chama cha upinzani CHADEMA, Daniel John na kujeruhiwa mwengine Reginald Mallya.

https://p.dw.com/p/2snY5
Dar es Salaam, Tansania Freeman Mbowe
Picha: DW/Said Khamis

J2.16.02.2018-US warns Tanzania about killings - MP3-Stereo

Pamoja na kuhimiza uchaguzi huru na wa haki katika uchaguzi mdogo hapo kesho nchini humo, taifa hilo pia limetaka uchunguzi ufanyike na wahusika wafikishwe katika vyombo vya sheria. DW imezungumza na mchambuzi wa siasa za Tanzania, mhadhiri wa zamani wa Chuo Kukuu cha Dar es Salaam, mwalimu Azavel Lwaitama na kwanza anaelezea onyo la Marekani kwa Tanzania litakuwa na matokeo gani.