1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa hali ya hewa.

Abdu Said Mtullya28 Aprili 2009

Marekani itashiriki katika kutayarisha mkataba mpya juu ya ulinzi wa mazingira.

https://p.dw.com/p/Hfh4
Waziri mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton asema Marekani itachukua hatua katika kulinda mazingira.Picha: picture alliance / landov

Baada  ya sera ya miaka  mingi ya kukwamisha juhudi, Marekani sasa inakusudia kushiriki katika harakati zinazoendeshwa duniani kote katika kukabiliana  na mabadiliko ya hali  ya hewa.

Serikali ya Ujerumani imetiwa moyo na mtazamo huo mpya wa Marekani.

Mtazamo huo mpya  umesisitizwa katika hotuba ya waziri  wa mambo ya nje wa Marekani bibi Hillary Clinton kwenye kongamano juu ya nishati mjini Washington.

Hizo zilikuwa habari za kufurahisha kwa waziri wa mazingira wa Ujerumani Siegmar Gabriel.

Waziri Gabriel amesema viongozi  wa siasa  nchini Marekani sasa wanajizatiti katika ulinzi wa hali  ya  hewa. Waziri huyo ameeleza kuwa hayo hayakuonekana katika minne iliyopita.

Waziri Gabriel amesema utawala wa rais Obama umeamua kuwa na msimamo tofauti na ule wa utawala wa rais Bush juu  ya suala la ulinzi wa mazingira.

Waziri wa Ujerumani  amesema mtazamo mpya wa Marekani  juu ya ulinzi wa mazingira siyo kauli tupu.

Msimamo huo ulisisitizwa  na waziri  wa mambo ya nje wa  Marekani Hillary Clinton kwenye kongamalo juu ya nishati mjini Washington.

Bibi Clinton aliwaambia  wajumbe kwamba mabadiliko ya hali ya hewa ni hatari ya kweli kwa dunia na lazima hatari hiyo ikabiliwe haraka. Amesema rais Obama na timu  yake yote wapo tayari kuikabili  changamoto hiyo.

Bibi Clinton ameeleza wazi kuwa Marekani haitajiweka kando tena.Amesema rais Obama na yeye mwenyewe wanaliweka suala la ulinzi wa hali ya hewa kwenye kitovu cha sera za nje za Marekani.

Mwandishi/Mtullya

Mhariri/Abdul-Rahman