Marekani na Urusi yabadilishana mawakala wa ujasusi | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 10.07.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Marekani na Urusi yabadilishana mawakala wa ujasusi

Urusi na Marekani zimetekeleza mabadilishano makubwa ya majasusi tangu kumalizika kwa vita baridi, yaliyofanyika katika uwanja wa ndege wa Vienna , nchini Austria.

Ndege ya Marekani , mbele, na nyuma ni ndege ya Urusi , zinazoaminika kuwabeba mawakala wa ujasusi ambao nchi hizo zimebadilishana mjini Vienna.

Ndege ya Marekani , mbele, na nyuma ni ndege ya Urusi , zinazoaminika kuwabeba mawakala wa ujasusi ambao nchi hizo zimebadilishana mjini Vienna.

Moscow.

Urusi na Marekani zimetekeleza mabadilishano makubwa ya majasusi tangu kumalizika kwa vita baridi, yaliyofanyika katika uwanja wa ndege wa Vienna, nchini Austria. Ndege moja iliwaleta mawakala 10 wa Urusi walioachiwa kutoka Marekani baada ya kikao cha mahakama , ambapo walikiri kufanya upelelezi wa kijasusi. Ndege nyingine iliripotiwa kuwa na watu wanne ambao walihukumiwa kufanya ujasusi nchini Urusi, ambao wamepewa msamaha wa rais baada ya kutia saini taarifa kuwa wana hatia. Mmoja kati ya wale waliohusika katika ubadilishanaji huo, ni mtaalamu wa masuala ya kinuklia Igor Sutyagin ambaye alifungwa jela nchini Urusi mwaka 2004. Kaka yake Dmitry amesema kuwa Igor atawasili nyumbani hivi karibuni. Tukio lote hilo limekamilika haraka , hali inayoashiria kuwa Urusi na Marekani zote zina nia ya kuepusha athari katika uhusiano wao.

 • Tarehe 10.07.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OFiI
 • Tarehe 10.07.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OFiI
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com